Wakati rais jakaya kikwete akisuasua
kuwachukulia hatua viongozi
waliotajwa na bunge kuhusika katika
wizi wa zaidi ya bilioni 320 kwenye
akaunti ya tegeta esrcow
Mbunge
wa kigoma kusini david kafulila
ameibuka upya na ameivaa ikulu
Baada ya kusema ikulu ya rais jakaya
kikwete inamedhamilia kuwalinda wezi
waliohusika katika kuiba pesa
hizo
Baada ya kumzuia mkurugenzi wa
ofisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa pccb dk edward hosea
kutoiwasilisha taarifa ya uchunguzi
juu ya sakata hilo la esrcow kwa
umma kutokana na ripoti ya pccb
kuwataja vigogo wa ikulu kuhusika
katika kuchota pesa kwenye benk ya
stabink.
Hayo yamebuliwa mda huu jijini dar es
salaam na mbunge wa kigoma kusini
david kafulila wakati wa mkutano na
waandishi wa habari ambapo kafulila
huku akizungumza kwa uchungu alisema
inasikitisha kuona jinsi ikulu
inavyotumia ubabe wake kumzuia dk
hosema kutoiweka wazi ripoti yake ya
uchunguzi.
“tunafahamu wazi serikali inataka
kuwalinda watu waliochota
pesa,kutokana na kitendo chake
kumzuia pccb asiweka hadharani ripoti
kwa kisingizia uchunguzi
ujakamilika,ujakamilika kivipi wakati
tunakumbuka wazi mkurugenzi wa pccb
dk hosea wakati kongamano la sadc
kuhusu rushwa uliofanyika mkoani
mwanza mwezi novemba”
“alisema ripoti yake ya uchunguzi
kuhusu akaunti ya escrow umekamilika
na tayari wameshamkabidhi waziri mkuu
ingawa waziri huyo mkuu alikana,na
hii yote inafanyika hivi ni kutokana
na ripoti ya pccb kuwepo na majina
ya vigogo wa ikulu ambao walichota
pesa kwenye benki ya stabink” alisema kafulila
Kafulila aliongeza kuwa leo majina ya
watu waliochota pesa kwenye benki ya
mkombozi tu wanatajwa ,huku wengine
kwenye benki ya stabink benki
wakiachwa kwa kuwa ni vigogo wa
ikulu.
“leo majina ambao kamati ya pac
waliyopewa na pccb ni ya benki ya
mkombozi huku majina ya benki ya
stabink ambao watu walichota pesa kwa
maboksi,sandalusi,magunia ambao wengi
wao ni vigogo wakubwa wa ikulu
wakiachwa,na ndio maana ikulu hii
inakataza ripoti ya pccb iwekwe wazi
kwakuwa itaweza kuvuruga nchi
kwasababu wahusika waliochota pesa
wengi ni watu wa ikulu”aliongeza
kafulila.
Kuhusu jeuri ya mmiliki wa IPTL,Bwana Seith
Kafulila ambaye pia ni katibu mwenezi
wa chama cha NCCR MAGEUZI alisema
jeuri aliyekuwa nayo Bwana Seith kwa
kuzivimbia mamlaka zote ikiwemo
mamlaka ya ukusanyaji kodi tra
inatokana na kigogo huyo kufahamu
wizi huo ameufanya na vigogo wa
kubwa wanchi.
“huyu bwana seith anakuwa jeuri sana
kwakuwa anauhakika pesa za escrow
amekula na wengi hata akifanya jambo
anajua wazi hakuna wakumchukulia
hatua kwakuwa wako wengi, na hii
inatokana kutokuwa na serikali makini
ndio maana inamuacha huyo taperi
kufanya anavyotaka ila serikali ijue
huyo mtu avyojisifu hivi
atakujakuleta machafuko
nchini”alitabainisha kafulila.
Katika hatua nyingine mbunge huyo wa
kigoma kusini alisema kwa sasa chama
chake cha NCCR MAGEUZI kwa kushirikiana na
umoja wao wa vyama vya upinzani
nchini waanza rasmi kwenda kwa
wananchi kuwaeleza kuhusu suala nzima
lilivyo la escrow na wamepanga kuanza
na mkoa wa kigoma.
“tunaanza tena ziara mkoani kigoma
kuhamasisha umma uelewe kuhusu
ufisadi huu,na tunatawajulisha
watanzania kuwa ccm haina uhalali wa
kuchaguliwa kwasababu imeshindwa
kuisimia serikali yake kwani makam
mwenyekiti taifa na katibu wa ccm
wamesisitiza kuwa wahusika wawajibike
lakini wamegoma”alisema kafulila.
0 comments:
Post a Comment