
Miss South Africa Rolene Strauss 
ameibuka mrembo wa dunia wa mashindano ya Miss World 2014, akiwashinda 
zaidi ya warembo 120 katika shindano lililofanyika jijini London, 
Uingereza.
Mshindi huyo wa shindano la Miss World 2014 alivikwa 
taji la urembo na mshindi wa Miss World 2013, Megan Young kutoka 
Ufilipino na kushangiliwa na mshindi wa pili na wa tatu, ambao ni Miss 
Hungary Edina Kulcsár na Miss Marekani Elizabeth Safrit. Kwa mujibu wa 
ukurasa rasmi wa mtandao wa Internet, mshindi huyo mwenye umri wa miaka 
22 ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya udaktari na anafurahia 
kucheza michezo ya golf, netboli na kuendesha baiskeli na kujisomea 
vitabu vya burudani na elimu.Washindi wa tano wa mwanzo katika mashindano ya urembo ya mwaka huu walikuwa kutoka Uingereza, Marekani, Hungary, Australia na Afrika Kusini.
Shindano la Miss World 2014 pia lilikuwa na mshindano tanzu na mataji mengi, ambayo yalifanyika kuelekea siku ya fainali kuu.
Kwa mara ya kwanza, washindani watano walitangazwa kuwa Warembo wa Miss World 2014 wenye Lengo: Washindi hao ni Miss India, Miss Kenya, Miss Brazil, Miss Indonesia and Miss Guyana.
 





 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment