Baada ya kufanya show  Freedom City
 Mall nchini Uganda iliyokuwa na mafanikio makubwa weekend iliyopita 
nchini Uganda, Davido aliombwa kuhudhuria Laftaz iliyopo Centenary Park 
siku ya jumatatu usiku kwa ajili ya usiku wao wanaouita "Drunken 
Monday", usiku ambao unajuisha members wa team no sleep. 
Dili hilo 
lilisimamiwa na Pallaso ambae amefanya collable na Davido na muimbaji 
huyo alitokea akiwa na Davido ambae alikuwa amevaa jezi ya Cranes ya Uganda.
Kila kitu 
kilienda sawa, alipiga picha na mashabiki zake mpaka pale Dj wa sehem 
hiyo alipopiga wimbo wa Diamond  "Number One Rmx" aliomshirikisha 
Davido,
Davido 
alibadilika na kuondoka sehem hiyo huku akitoa maneno machafu. Licha ya 
kubembelezwa na meneja wa Hangout lakini Davido hakutaka kusikia 
chochote na kuondoka haraka kuelekea katika hoteli aliyofikia.
Mtandao wa 
matookerepublic umeripoti kuwa Davido ameuga na kuwa adui wa Diamod 
baada ya tuzo za Channel O Davido alipoondoka mikono  mitupu na Diamond 
kubeba tuzo 3. Davido amehisi kudharauliwa kwasababu Diamond kashinda 
tuzo kwa original version ya Number one huku Davido akihisi kuwa remix 
ya wimbo huo ndio umeufanya kuwa maarufu 

 





 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment