Facebook

Wednesday, 3 December 2014

WARIOBA: RIPOTI YA ZITO DHAIFU, NGELEJA KAHUSIKAJE ESCROW?

Waziri mkuu na makamu wa pili wa rais wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema ripoti ya kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) chini ya Kabwe Zitto kuhusu akaunti ya tegeta Escrow ilikuwa dhaifu, yenye kuendeleza tabia ya kulindana.

Zaidi ya hapo, Jaji Warioba alisema kwa namna fulani Bunge la Jamhuri ya Muungano limeingilia uhuru wa mihimili mingine kutokana na maazimio yake.

Akizungumza na Raia Tanzania ofisini kwake jijini Dar es salaam, Jaji Warioba alisema ripoti ya PAC imeacha maswali kadhaa bila majibu.
"Wameacha maswali hayana majibu, la kwanza, taarifa ya kamati ya Hesabu za serikali (PAC), imeonyesha  udhaifu katika maeneo mengi. Moja ni katika eneo linalohusu  Wizara ya Nishati na Madini, pili ni yale yanayohusu Wizara ya fedha na tatu ni yale yanayohusu Wizara ya Viwanda na Biashara.

Alisema katika mjadala wa sakata la Escrow Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara hazikuguswa licha ya kwamba ndio wahusika wakuu wa hasara inayojulikana.

" Katika mawasiliano yote (kuhusu utoaji fedha Escrow) Waziri mkuu walimuingiza kwa kusema alikuwa akipata nakala za barua lakini wizara ya Fedha ilihusika katika mawasiliano na wameachwa" alisema Warioba.

Yafuatayo ni maelezo ya kina ya Jaji Warioba:

IPTL NI MZIGO

"Nataka nizungumzie mchakato wa Escrow, kwanza, IPTL imekuwa mzigo kwa nchi kwa muda mrefu tangu kampuni hiyo ilipoundwa, imekuwa na matatizo mengi. Katika kipindi hicho nchi imepoteza fedha nyingi kupitia kesi zilizotokana na IPTL ".

Nimesikia kwenye bunge kampuni moja ya wanasheria imelipwa sh.bilioni 62 lakini haikuwa peke yake, katika kesi hizo kulikuwa na gharama za TANESCO kwa kuwa walikuwa wakipeleka watu na kulikuwa na gharama za serikali, kwa hiyo fedha zilizotumika kwa migogoro hii ni nyingi.

"Katika utendaji wenyewe kulikuwa na matatizo, kwa hiyo nadhani ni jambo jema kwa sababu ya tatizo lililotokea lizungumzwe kwa undani ili kumaliza matatizo ya IPTL, tusiendelee nayo na gharama zake kwa nchi..
Kwa hiyo kulipeleka bungeni ilikuwa ni jambo zuri na limezungumzwa na ninaamini baada ya mchakato huu tutafika mahali tumalize matatizo ya IPTL na kuendelea na shughuli zingine za uchumi" alisema Warioba.

MAMBO MATATU MUHIMU

Warioba alisema hadi suala la IPTL linafikishwa bungeni na kisha kupatikana  kwa maazimio ya Bunge kuna mambo matatu yameongoza mjadala:

La kwanza, ni wananchi, wananchi walikuwa na hamu ya kusikiliza mjadala Hui na kuona matokeo yake ni nini. Yalipokuwa yakitokea matatizo kama vile ya umeme, walikuwa wakilalamika kwa kuwa walitaka wafuatilie kwa ukaribu sana.

Hili kwa kiwango kikubwa naweza kusema ni kama vile imani ya wananchi kwa uongozi, hivyo kwa kila jambo linalotokea likiwahusu viongozi, wananchi wanakuwa makini kuona ni nini kitatokea. Hivyo bunge lilipokuwa likizungumza walijua kwamba wananchi wanatarajia kutatokea uamuzi mzito na si mazungumzo tu.

La pili, ni kwamba tunazungumza wakati huu ni kama wahisani wamesimamisha misaada kwa serikali na hata katika mjadala wengine walitaja hilo, kwamba limetuletea matatizo nchi sasa haipati misaada, kwa hiyo walipozungumza walijua kuwa wahisani walitaka waone matokeo ya hilo.

La tatu, nadhani ni siasa kwa kiwango kikubwa. Tunaingia katika kipindi cha uchaguzi, kwa hiyo vyama vinatafuta mambo ya kampeni kwa pande zote mbili, chama tawala na vyama vya upinzani. Nina hakika hili litaendelea kuwa jambo litakalozungumzwa wakati wa kampeni, kwa hiyo mazungumzo yote, huo ndo ulikuwa msingi wake.

FEDHA ZA ESCROW NI ZA NANI?

Mazungumzo yalivyokwenda utaona kubwa ambalo ndilo msingi wa uamuzi uliofanywa na bunge ni kuwa fedha za Escrow zilikuwa mali ya umma na ndivyo wananchi wamefanywa waamini hilo lakini hakuna palipothibitishwa kuwa ni za umma. Msingi wa Escrow ni kwamba pande hizi mbili hazikuwa zikikubaliana kuhusu capacity charge, hivyo kwa kuwa hawakuwa wakikubaliana waliona wawe na utaratibu, kwanza waendelee kushauriana wao wenyewe au kwenye mahakama ya nje; lakini kwa kipindi hicho kwa kuwa hawakuwa wakikubaliana, iliafikiwa kuwe na mpango wa kuweka fedha mpaka watakapofikia makubaliano. Katika kipindi chote hicho IPTL ilikuwa ikitoa huduma, kwa hiyo kwa vyovyote vile ilikuwa na haki ya kulipwa capacity charge watakapokubaliana.

Hivyo kilicho cha uhakika katika fedha zile ni kwamba, zipo za capacity charge, hawakufika mahali waseme ni kiasi gani, lakini kwa kuwa sasa wanakwenda kuchunguza nina hakika mwisho itaonekana sehemu kubwa ya fedha hizo zilikuwa ni za capacity charge", alisema warioba.

Hata hivyo, wananchi wamefanywa waamini kwamba fedha zote zilikuwa ni za umma, hilo ni mwelekeo wa kisiasa. Ni sawa wamefikia hapo, kama wameamua kwa msingi huo, wanasema kuna watu ni lazima wawajibike kwa hasara ambayo nchi imepata.

VIPORO VYA MASWALI

Jaji Warioba alisema mchakato huu wa IPTL na akaunti ya Escrow umeacha maswali kadhaa.:

" Wameacha maswali hayana majibu, la kwanza , taarifa ya kamati ya Hesabu za serikali (PAC), imeonyesha udhaifu katika maeneo mengi. Moja ni katika eneo linalohusu Wizara ya Nishati na Madini, pili ni yale yanayohusu Wizara ya ya Fedha na tatu ni yale yanahusu Wizara ya viwanda na biashara.

" Hasara inayotajwa kwa uhakika ilikuwa inahusu kodi inayotokana na mauzo ya hisa na hiyo si strictly ya Escrow  ni kodi ya mauzo ya hisa , kwa namna ya capital gains tax na stamp duty. Wanaohusika hasa ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na pia wizara ya viwanda kwa maana ya Brela.

"Katika mjadala huu inaonekana kama wizara ya fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara hazikuguswa na huko ndiko yametokea matatizo ya hasara inayojulikana. Nimesoma taarifa ya PAC, wakifika kwenye wizara ya fedha, wanasema PAP kwa kushirikiana na maofisa wadogo wa TRA walofanya dhambi hii, sasa ni kama wanataka kuilinda Wizara ya Fedha. Katika mawasiliano yote Waziri Mkuu walimuingiza kwa kusema  alikuwa akipata nakala za barua kakini Wizara ya Fedha ilihusika kabisa katika mawasiliano na wameachwa.

Brela wamefanya uzembe kwamba, unaweza kuandikisha kampuni na watu wakatia saini na majina hayapo, unaona kulikuwa na kasoro lakini haikuguswa. Kwa hiyo licha ya kuwa wameamua kuchagua watu waliohusika, inaonekana walikwenda mahali pamoja na huku kwingine wamewalinda.

Wamewalinda viongozi wa wizara ya fedha na Wizara ya Viwanda, wakati vitendo vilivyosababisha  hasara ya kodi kupatikana vimetendwa katika wizara hizi. Nijachouliza hapa ni kwa nini hawakutajwa, kuna element ya kulindana.

La pili linaloonekana kwamba kuna kulindana ni kwamba, waliopokea fedha kutoka kwa Rugemalira (James) wote wametajwa. Akaunti ya Rugemalira imetajwa katika benki ya mkombozi na hao wametuhumiwa lakini wanaohusika na fedha zilizotolewa stanbic bank , ambazo  kamati inasema zilichukuliwa kwenye mifuko ya rambo, lumbesa na kwenye magunia, hawakutaja ni nani alichukua.

"Kwa sababu kama wanajua zilichukuliwa kwa njia hiyo, lazima watakuwa wanajua ni nani alichukua. Hivyo ni kwa nini hao waliochukua upande huu hawakutajwa? Unaaanza kuwa na maswali kuwa hapa kuna dalili za kulindana na wameendelea hivyo na kutoa uamuzi.

"Umuzi ule ni kama wa mahakama, bunge limekaa na kuamua kwamba fedha hizi na hasa alizolipa Rugemalira zilikuwa chafu na wote waliopokea fedha hizo walizipokea zikiwa chafu, hivyo na wao waadhibiwe. Wana ushahidi gani? Hawakuwasikiliza wale watu. Unasema kuna askofu amepewa fedha umuhukumu kwamba alijua kuwa ni fedha chafu, kuna jaji hapa alipata fedha  unasema alijua ni fedha chafu, kuna Waziri alichukua fedha unasema alijua kuwa ni chafu, lakini hawakuwasikiliza.

" Kwa hiyo, wamehukumu bila kuwasikiliza na wamependekeza hatua za kuchukua. Baadhi yao wamesema wachukuliwe hatua za kinidhamu na wengine walipe kodi. Najiuliza kama askofu amepewa fedha, unasimama kwenye bunge unasema ajiandae kulipa kodi, najiuliza hivi ni mara ya kwanza kwa wao na watu wengine kupata fedha za aina hii? Mbona viongozi hao hao wanatoa misaada tena mikubwa na mahali pengi, mamilioni hatujasikia wakisema waliopewa walipe kodi.

" Hivi tuna uhakika gani kwamba hizi site zinazochangwa ni halali? Kwanini hawa ndio walipe kodi lakini zinazotolewa

0 comments:

Post a Comment