
Mwanamme mmoja raia wa Uturuki 
aliyempiga risasi na nusura amuue aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki 
papa John Paul wa pili mwaka 1981 ameweka maua kwenye kaburi lake katika
 makao makuu ya kanisa katoliki ya Vatican.
Bwana Agca aliomba kukutana na kiongozi wa sasa wa kanisa katoliki papa Francis lakini hata hivyo ombi lake lilikataliwa
Aliachiliwa kutoka gerezani nchini Italia mwaka 2000 na kisha baadaye akatumikia kifungo chengine cha miaka 10 nchini Uturuki kwa makosa tofauti.
Hadi sasa sababu zake za kutaka kumuua papa John Paul hazijulikani.
 





 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment