|
Google Inc ni moja kati ya kampuni nguli na tajiri sana mtandaoni. Google inapenda sana kucheza na vitu na kubuni mambo mapya kupitia vitu hivyo hasa kiteknolojia. inasemekana pengine ndio kampuni kubwa ya kiteknolojia inayoongoza kwa ubunifu. Licha ya kuwa mafanikio makubwa kampuni hii ina mambo mbalimbali yanayovutia na kufurahisaha. Leo nitakuonesha baadhi ya mambo ya kufurahisha unavyoweza kuyafanya kupitia Google Search. 1. FANYA PAGE IZUNGUKE KAMA PIPA Ukiingia katika ukurasa wa google na ukitafuta ‘DO A BARREL ROLL’ page yote itazunguka nyuzi 360 2. GOOGLE YA MWAKA 1998 Ukitaka ona jinsi google ilivyokua mwaka 1998 basi tafuta ‘ GOOGLE IN 1998‘ katika ukurasa wa google na utaona muonekano wake kwa mwaka huo jinsi ulivyokuwa 3. ATARI BREAKOUT Katika ukurasa wa Google tafuta ‘ATARI BREAKOUT‘ kisha yatatokea majibu baada ya hapo bonyeza ‘IMAGES’ litatokea gemu la kubomoa matofari kwa kutumia ki mpira kidogo unaweza ukalicheza gemu hili. 4. ZERG RUSH Ukiandika neno ‘ZERG RUSH‘ katika ukurasa wa google , yatakuja majibu vizuri kisa utashangaa vinatokea vi O vingi viingi chini na juu ya kompyuta. vitaanza kula maneno yote yaliyo jitokeza katika hiyo page kama majibu. ili kuviua vi O hivi inabidi uvibonyeze na Mouse mara 3 kwa mkupuo 5. MVUTONO Katika Sehemu ya kutafuta vitu katika page ya google andika ‘Google Gravity’ kisha bonyeza ‘I’m Feeling Lucky’ ukisogeza Mouse tuu utaona maneno yaanza kudondoka chini ya skrini yako kuonyesha nguvu za mvuta 6. JIPANGIE MUDA/DAKIKA Hii pia inavutia. hivi unajua unaweza kujipangia muda katika ukurasa wa google? ndio unaweza mfano ukiandika ‘SET TIMER FOR 10:30PM‘ inamaanisha hapa ikifika saa nne na nusu usiku kompyuta yako itapiga kelele/mlio kukukumbusha kuwa mda huo umefika, kama alarm/kengere tuu sio? 7. TAFUTA KWA SAUTI/KUTAMKA Sio lazima kila unachokitafuta lazima ukiandike, unaweza pia ukakitafuta kwa kutumia sauti yako. jinsi ya kufanya hvyo, Ingia katika ukurasa wa google alafu tafuta kialama cha kipaza sauti, mara nyingi kinakua mwishoni mwa upande wa kulia katika sehemu unayoandika kitu unachotaka kukitafutakibonyeze kile kisha unaweza sema kitu unachotaka kukitafuta. 8. VITABU Kama wewe ni mpenzi sana wa vitabu na unapenda soma basi kuna njia rahisi ya kuvipata. Ingia google sehemu ya kutafuta, Andika ‘BOOKS BY‘ kisha jina la mwandishi au mtunzi, Hapo vitatokea vitabu vyo vya huyo mwandishi/mtunzi 9 .SINEMA Ukiachana na vitabu, je wewe ni mpenzi wa sinema? basi hili litakusaidia pia. ingia ukurasa wa google kisha andika jina la mwigizaji ikifuatiwa na neno ‘MOVIES‘ hapo zitatikea sinema za huyo msanii kisha utachagua chaguo lako 10. GOOGLE KAMA KIOO Hii pia ni ya kushangaza, Google inaweza kuwa kama kioo. hii inamaanisha ukiandika maneno yatakua yanaonekana kama yako ndani ya kioo yaani yatakua yamejigeuza, yanaanza kulia yanaenda kushoto. kuona mfumo huu wa kioo bofya hapa Hayo ndio mambo 10 ambayo unaweza fanya ukiwa katika tovuti ya www.google.com kwa kumpyuta na mengine ata kwenye simu-janja(SMARTPHONE, mambo haya ni ya aina yake na ya kushangaza kwa sababu tovuti nyingi hazina ubunifu kama huu. Google bado ipo katika zile kampuni zenye maendeleo sana katika masuala ya teknolojia na inatoa changamoto kwa makampuni mengine kama Apple. Je uzi huu umekusisimua, tuambie ni kipi umekifurahia zaidi?
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na teknolojia.
|
0 comments:
Post a Comment