Mtandao wa kijamii wa Instagram umetangaza rasmi kufikisha watumiaji milioni 300 na hivyo kuipita kwa mbali zaidi mtandao Twitter wenye watumiaji milioni 284.
Akiongea kwenye kipindi cha Newsbeats 
mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Kevin Systrom akiri kukua zaidi kwa 
mtandao wake huo wa kijamii kutokana na kutumiwa 
zaidi na makampuni na watu binafsi kusambaza taarifa kwa kwa jamii kwa 
njia ya picha.Kitu kingine kinachofanya mtandao  wa Instagram kukua 
zaidi ni baada ya kununuliwa na Facebook
 yenye watumiaji bilioni 1.35 mwaka 2012.Instagram uthibitisha akaunti 
za makampuni,watu maarufu na wanamichezo imesababisha kuifanya iweze 
kupendwa zaidi na watu wa rika zote kote Duniani. 
Mkurugenzi huyo pia aelezea jinsi wanavyokabiliana na akaunti bandia kwa kuzifuta mara moja na pia kuwa na mpango wa kuanzisha kipengele kipya kwa ajili ya matukio.
Mkurugenzi huyo pia aelezea jinsi wanavyokabiliana na akaunti bandia kwa kuzifuta mara moja na pia kuwa na mpango wa kuanzisha kipengele kipya kwa ajili ya matukio.

0 comments:
Post a Comment