Ngugi wa Thiong’o ametunukiwa shahada ya Udaktari
wa heshima na Chuo Kikuu cha Bayreuth cha
Ujerumani, huku vitabu vyake “Shetani Msalabani” na
“Matigari” vikiwa vimempatia umashuhuri na
mashaka pia nchini mwake.
Hakuna anaetunukiwa tuzo ya udaktari wa heshma
bila ya kuistahiki. Na Ngugi wa Thiong’o,mwandishi
vitabu na mtaalam wa fasihi amefanya mengi
yanayostahiki tuzo hiyo.Kitabu chake
kilichochapishwa mwaka 1964 kwa kiingereza “Weep
Not,Child” au kwa kiswahili “Usilie mtoto” kilikuwa
kitabu cha kwanza kuchapishwa kwa Kiingereza na
mwandishi vitabu kutoka Afrika Mashariki.
Ngugi wa Thiong’o amesomea katika chuo kikuu
maarufu cha Uganda,Makerere, na pia mjini Leeds
nchini Uingereza.
Baadae aliamua lakini kuandika vitabu vyake kwa
lugha yake ya mama tu,”kikikuyu”.Sababu za
kutafakari lugha gani itumike ameitaja Ngugi wa
Thiong’o katika mahojiano na DW alipoelezea uamuzi
wa kuandika mchezo wa kuigiza pamoja na mtunzi
mwenzake katika mwaka 1976,Ngugi wa Mirii,na
kusema: “Pekee ukweli kwamba tulibidi kujiuliza
michezo ya kuigiza tuiandike kwa lugha gani,inatoa
picha ya jinsi tulivyogeuka kuwa wageni katika nchi
yetu wenyewe kwasababu suala hapo lilikuwa dhahir
nalo ni kwamba tuandike lugha inayozungumzwa na
walio wengi.”
Lugha ya kikikuyu inazungumzwa na zaidi ya watu
milioni sita nchini Kenya na ndio lugha ya mama ya
Ngugi wa Thiong’o na mtunzi mwenzake Ngugi wa
Mirii.
Ngugi wa Thiong’o ameshawahi kufungwa
Kitabu cha mchezo wa kuigiza kilichopewa jina
“Ngaahika Ndeenda” au kwa kiswahili “Nitaowa
wakati nnaotaka” ingawa kilimpatia umashuhuri
mkubwa lakini pia kilimpatia mashaka kutoka
serikalini.Kitabu hicho kilipigwa marufuku na
mwenyewe Ngugi wa Thiong’o kuwekwa korokoroni
kwa muda wa mwaka mmoja.
Lakini kifungo hicho kilimzidishia nguvu za
kuendelea kuandika kwa lugha ya kikikuyu.Huko
huko jela aliandika kitabu chengine akitumia karatasi
za chooni.
Ngugi wa Thiong’o ameshawahi kutunikiwa vyeo
kadhaa vya udaktari wa heshima.
Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha zaidi ya 40.
Katika hati ya kupatiwa shahada hiyo ya udaktari wa
heshima,chuo kikuu cha Bayreuth kinasifu” mchango
wake mkubwa unaostahiki kusifiwa wa kueneza
fasihi ya kiafrika na hasa fasihi kwa lugha za
kiafrika.”Vitabu vyake ni msingi wa matumaini ya
mageuzi katika uhusiano kati ya Afrika na sehemu
nyengine za dunia”-imeandikwa ndani ya hati ya
shahada ya udaktari wa heshima ya chuo kikuu cha
Bayreuth kwa Ngugi wa Thiong’o.
0 comments:
Post a Comment