Ukiachana na Tuzo za Grammy ambazo zitafanyika mwakani February 2015.Hii ni orodha ya albamu ambazo zimetajwa kufanya vizuri sokoni kwa mwaka 2014

Dada lao, Bey alifanya vizuri kwenye soko kutokana na mafanikio aliyoyapata kupitia album aliyoiita jina lake, wenyewe wanaiita ‘self titled album‘, ikiwa na nyimbo kali kama ‘Drunk in Love’ aliyofanya na mumewe, Jay Z.

Ukiachilia mbali zile noma za kukaa jela, kuzinguana na mpenzi wake Karrueche, Mahudhurio ya Mahakamani na zile adhabu za Huduma za Kijamii ambavyo vimemuweka busy mwaka mzima, ‘X’ album ya Chris Brown iliyobebwa na ‘Loyal’ na ‘Fine China’. Mauzo yake wiki ya kwanza ilikuwa copy 146,000 huku kukiwa na fununu kwamba staa R. Kelly ni kama aliweka nguvu hivi kuproduce nyimbo kadhaa kwenye albam hii.

Sidhani kama lebo ya Rapa T.I, Hustle Gang wanajutia nguvu waliyoiweka kumsimamisha Iggy kutokana na mafanikio ambayo kayaonyesha mpaka sasa, tukianza na ule ushahidi wa Tuzo aliyoipata ya Favorite Rap/Hip Hop Album katika Tuzo za American Music Awards 2014.

Msaada wa wakali kama producer Timberland na L.A Reid wakaweza kuzirudia baadhi ya nyimbo za Hayati MJ alizorekodi kuanzia mwaka 1983 mpaka 2001 kumefanya Dunia ipokee vizuri album yake ambayo imefanya mauzo ya copy zaidi ya mil.1 duniani kote mpaka sasa.

‘Because I’m Happy’ hakuna ambaye hakufurahishwa na kazi hii nzuri ya Pharrell kutoka kwenye albam yake ya GIRL, ameshakusanya tuzo nyingi lakini
moja kati ya kubwa ni ile ya kupata kutambulika kuwa ‘Hollywood Walk of
Fame’ na bado anawania tuzo nyingine 6 kwenye Tuzo za Grammy.

Mbali
ya ugeni wake kwenye masikio na macho ya watu, haikuwa rahisi kupenya
na kukubalika lakini tayari kapita na moja ya mafanikio ambayo
yanazungumziwa ni yale ya Sam Smith kutajwa kuwania tuzo nyingine sita pia za Grammy, pamoja na wakongwe kama Pharrell na Beyonce.

‘Stronger’ ya Tank
imeonyesha ile nguvu ambayo anayo baada ya kutoonekana kwenye climax ya
muziki kwa kipindi kirefu akijihusisha na masuala mengine ikiwemo
kucheza movie, album hii imetajwa kushika nafasi ya 13 kati ya album 200
bora za Billboard.
0 comments:
Post a Comment