Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal amesema wachezaji wake wawili walikataa kupiga penati ya kwanza katika mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Argentina katika Kombe la Dunia.
Beki Ron Vlaar alijitolea kupiga penati hiyo ya kwanza ambayo ilizuiwa na kipa wa Argentina Sergio Romero.
Kipa huyo "alifundishwa jinsi ya kudaka penati" na Van Gaal, wakati akiifundisha AZ Alkmaar.
"Niliwaambia wachezaji wawili wakapige penati ya kwanza, kabla ya Vlaar
kujitolea" amesema meneja huyo mpya wa Manchester United.
Argentina walishinda 4-2, Romero akipangua penati mbili
Argentina walishinda 4-2, Romero akipangua penati mbili
0 comments:
Post a Comment