Patrice Evra ameomba kuondoka Manchester United, ingawa hajawasilisha ombi rasmi la uhamisho.
Juventus wamekuwa wakimuulizia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Evra, 33, alitia saini mkataba wa mwaka mmoja zaidi Old Trafford.
Hata hivyo mchezaji huyo amewasiliana na maafisa wa United kuulizia uwezekano wa kuhamia Italy, na uhamisho huo huenda ukatokea siku ya Alhamisi.
Evra alijiunga na Manchester United kwa pauni milioni 5.5 akitokea Monaco January mwaka 2006.
Amecheza mara 379, akishinda makombe matano ya Ligi Kuu ya England, na Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2008.
Ilidhaniwa angechukua unahodha wa Manchester United baada ya kuondoka kwa Nemanja Vidic.

0 comments:
Post a Comment