Baada ya kuteuliwa kwa mara ya pili kuinoa timu ya taifa ya Brazil "SELECAO".
Dunga,ameteua kikosi cha wachezaji 22 kitakachovaana na Colombia huko Miami nchini Marekano mnamo September 5 mwaka huu.
Na baada ya hapo siku nne baadae itavaana na Ecuador huko New Jersey katika Gillette Brasil Global Tour
Katika kikosi hicho Dunga amewajimuisha wachezaji mbalimbali ambao hawakuitwa katika kikosi kilichoshirili fainali za Kombe la dunia.
Dunga amewajumuisha wachezaji wawili mahiri kutoka Fc Porto ya nchini Ureno;Danilo na Alex Sandro.
Vilevile kamuita Rafael Cabral kutoka klabu ya Napoli na kiungo wa Corinthians Elias.
Nyota wawili kutoka Cruzeiro Ricardo Goulart na Everton
Ribeiro wameitwa kwa mara ya kwanza timu ya taifa baada ya kufanya vizuri katika Ligi kuu ya nchini Brazil "Brasileirao" msimu uliopita na kufanikiwa kunyakua Ubingwa wa Ligi hiyo.
Nyota wa Liverpool Philippe Coutinho na mchezaji mpya aliyesajiliwa na Chelsea Filipe Luis pia ni baadhi ya wachezaji walioitwa na Dunga kwa mara ya kwanza timu ya taifa Brazil alipoteuliwa kuwanoa Selecao .
Dunga ameongeza wachezaji wapya 10 kati ya 23 walionyanyaswa vibaya na Ujeruman katika nusu fainali waliyofungwa magoli 7-0 mwezi uliopita.
KIKOSI KAMILI
>MAGOLIKIPA
Jefferson (Botafogo)
Rafael Cabral (Napoli)
MABEKI
David Luiz (Paris Saint-Germain)
Marquinhos (Paris Saint-Germain)
Gil (Corinthians)
Miranda (Atletico Madrid)
Maicon (Roma)
Filipe Luis (Chelsea)
Alex Sandro (FC Porto)
Danilo (FC Porto)
VIUNGO
Luiz Gustavo (Wolfsburg)
Elias (Corinthians)
Fernandinho (Manchester City)
Ramires (Chelsea)
Willian (Chelsea)
Everton Ribeiro (Cruzeiro)
Oscar (Chelsea)
Coutinho (Liverpool)
WASHAMBULIAJI
Ricardo Goulart (Cruzeiro)
Hulk (Zenit)
Neymar (Barcelona)
Diego Tardelli (Atletico MG)
Imeandaliwa na........
Katemi Methsela
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata habari mbalimbali za michezo kwa muda muafaka.
0 comments:
Post a Comment