Kocha mpya wa Uholanzi, Guus Hiddink,
ameteua Kikosi chake cha kwanza tangu aanze
wadhifa huo kwa kuwataja Wachezaji Wanne
ambao hawakwenda huko Brazil kwenye Fainali
za Kombe la Dunia.
Wapya hao Wanne ambao wamo kwenye Kikosi
cha Wachezaji 25 ni Beki wa Stoke City Erik
Pieters, Rafael van der Vaart, Gregory van der
Wiel na Kipa Jeroen Zoet.
Wachezaji waliochwa kutoka Kikosi cha Brazil
kilichokuwa chini ya Louis van Gaal, ambae sasa
ni Meneja wa Manchester United, ni Jonathan De
Guzman na Terence Kongolo.
Hiddink atakipunguza Kikosi hicho na kubakisha
Wachezaji 23 mwishoni mwa Wiki ijayo na
Septemba 5 kitacheza Mechi ya Kirafiki na Italy
huko Bari na Septemba 9 kucheza Mechi yao ya
Kwanza ya Kundi lao la kufuzu EURO 2016 huko
Prague dhidi ya Czech Republic.
KIKOSI KAMILI:
Makipa:
Jasper Cillessen (Ajax Amsterdam), Tim
Krul (Newcastle United), Michel Vorm
(Tottenham Hotspur), Jeroen Zoet (PSV
Eindhoven)
Mabeki:
Daley Blind (Ajax Amsterdam), Stefan de
Vrij (Lazio), Daryl Janmaat (Newcastle United),
Bruno Martins Indi (FC Porto), Erik Pieters (Stoke
City), Gregory van der Wiel (Paris St Germain),
Paul Verhaegh (FC Augsburg), Ron Vlaar (Aston
Villa), Joel Veltman (Ajax Amsterdam)
Viungo:
Jordy Clasie (Feyenoord Rotterdam),
Nigel de Jong (AC Milan), Leroy Fer (Queens Park
Rangers), Arjen Robben (Bayern Munich), Wesley
Sneijder (Galatasaray), Rafael van der Vaart
(Hamburg SV), Georginio Wijnaldum (PSV
Eindhoven)
Washambuliaji:
Memphis Depay (PSV Eindhoven),
Klaas-Jan Huntelaar (Schalke 04), Dirk Kuyt
(Fenerbahce), Jeremain Lens (Dynamo Kiev),
Robin van Persie (Manchester United).
0 comments:
Post a Comment