Facebook

Friday, 22 August 2014

Unyama!! awachoma watoto wake mikono !


Watoto wanaodaiwa kufanyiwa ukatili wakionyesha vidonda
kwenye mikono yao ambavyo vinatokana na kuchomwa moto na
baba ya mzazi nyumbani kwao Mbagala Kibondemaji jijini Dar es
Salaam jana.


Vitendo vya ukatili dhidi yawatoto vinavyofanywa na baadhi
ya wazazi, vimezidi kukithiri nchini baada ya watoto wawili kudaiwa kuchomwa moto mi konona baba yao kwa kutumia tambi za jiko jijini Dar es Salaam. Katika tukio hilo, anayetuhumiwa
kufanya unyama huo ni Salum Juma, fundi gereji wilayani
Temeke, mkazi wa Mbagala Kibonde Maji, jijini Dar es Salaam.


Watoto hao mmoja mwenye umri miaka saba na mwingine miaka
mitano (majina yao yamehifadhiwa), akiwamo wa kumzaa na wa kufikia walikutwa na mkasa huo baada ya kwenda kuangalia runinga kwa jirani na kurudi nyumbani saa 5:00 usiku
Alhamisi wiki iliyopita.


Jirani yao, Omar Fusi, alidai watoto hao walieleza kuwa walichomwa na baba yao na kufichwa ndani,lakini baadaye majirani
waliwaona watoto hao wakiwa na majeraha.
Fusi alisema baada ya kuwaona wakiwa na majeraha, waliwahoji
ambapo walieleza kuwa walichomwa na baba yao baada ya kuchelewa kurudi kutoka kuangalia televisheni.


Kwa mujibu wa Fusi, kitendo hicho kilifanyika huku mama yao akiwa kwenye biashara zake za kukaanga mihogo.Fusi alisema baada ya kubaini
tukio hilo alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
wa Kibonde Maji ‘B’, Teofile Balae,ambaye alitoa taarifa kwa Ofi sa Ustawi wa Jamii kata ya Mbagala,Eliameresa Kaaya na kuripoti
polisi na kufanikisha baba huyo kukamatwa na kupelekwa katika
Kituo cha Polisi Maturubai ambako anaendelea kushikiliwa.


Badae alisema baada ya kushirikiana na Ofisa Ustawi wa Jamii na baba huyo kukamatwa, waliwachukua watoto hao na kuwapeleka Kituo cha Polisi Mbagala Kuu kwa ajili ya kupata fomu ya PF3 na kuwapeleka katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu kupatiwa matibabu.Mmoja wa wakazi wa eneo hilo,Erasto Kibara, alisema walibaini watoto hao kufanyiwa ukatili huo baada ya kumkuta mmoja wao adukani alikotumwa akiwa na majeraha na kumuuliza kilichompata kisha alitoa taarifa hizo kwa mwenyekiti wa mtaa
huo.
Ofisa Ustawi wa Jamii, Kaaya, akizungumza katika
Kituo cha Polisi Maturubai wakati watoto hao wakichukuliwa
maelezo na polisi, alisema kitendo wali chofanyiwa watoto hao ni cha kikatili na kuwataka wananchi kutoa taarifa pale wanapogundua ukatili katika mitaa yao ili kutokomeza vitendo hivyo vilivyoshika kasi nchini.

Chanzo chetu kiliwashuhudia watoto hao katika Kituo cha Polisi
Maturubai huku wakiwa na majeraha mkononi wakati
wakichukuliwa maelezo na maofisa wa polisi wa kituo hicho.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mbagala Rangi Tatu, Dk. Julius
Nyakazilibe, alithibitisha watoto hao kupokelewa hospitalini hapo
na kupatiwa huduma ya matibabu kutokana na majeraha yaliyosababishwa na moto.
 

“Ni kweli watoto hao tuliwapokea hapa hospitalini wakiwa na Ofisa Ustawi wa Jamii na wali patiwa matibabu,” alisema Dk.
Nyakazilibe
. Mama mzazi wa watoto hao, Christina Menasi, akiwa katika kituo cha polisi na mtoto wake mchanga huku akimnywesha uji, alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa katika biashara yake ya kuchoma mihogo na aliporudi nyumbani na kukuta hali hiyo, aliingiwa na hofu ya kuripoti tukio hilo kwa kumhofia mumewe.


Mama huyo alilaani kitendo hicho cha kikatili lakini alisema akifungwa yeye ndiye atakuwa na mzigo mkubwa wa kulea familia hiyo.
“Inatakiwa tuache vitendo hivi vya kikatili, lakini ikiwa mume wangu atafungwa, mimi ndiye nitakayebeba mzigo wa kulea hii
familia,”
alisema Christina. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya Kihenya,alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Maturubai na kwamba upelelezi unaendelea kabla ya kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

0 comments:

Post a Comment