Facebook

Sunday, 16 November 2014

Baada ya Simba kumkosa Simon Msuva yahamia kwa mdogo wake.

Baada ya kumkosa kiungo mshambuliaji wa
Yanga, Simon Msuva, Klabu ya Simba imehamia
kwa mdogo wake, James Msuva katika usajili wa
dirisha dogo linalofunguliwa leo.
Simba kwa kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya timu hiyo, Zacharia Hans Pope,
ilitangaza kutoa kiasi chochote cha fedha kwa
ajili ya kumsajili kiungo huyo mwenye kasi
katika kikosi hicho.
Usajili wa dirisha dogo unatarajiwa kufunguliwa
leo Jumamosi na kufungwa Desemba 15, mwaka
huu ukishirikisha klabu mbalimbali za ligi kuu.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani
ya uongozi wa timu hiyo, wamefikia hatua ya
kumsajili kiungo huyo baada ya benchi la ufundi
la timu hiyo ambalo lipo chini ya Mzambia,
Patrick Phiri na Selemani Matola kuridhishwa na
kiwango chake.

Chanzo hicho kilisema, Phiri ameridhishwa na
kiwango kikubwa cha kiungo huyo mwenye kasi
anayecheza namba saba kama anayocheza kaka
yake Simon baada ya kumuona kwenye mazoezi
ya timu ya vijana ya U-20.

“Uongozi umepanga kukutana na mdogo wake
Msuva (James) kwa ajili ya kuanza mazungumzo
ya timu hiyo kwa ajili ya kumsajili katika usajili
wa dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa
kesho (leo).
“James yupo anaichezea timu yetu ya vijana ya
U-20, akiwa hana mkataba wa kuichezea Simba,
hivyo tumefikia hatua ya kumsajili kwa mkataba
na kumpandisha kwenye timu ya wakubwa, hivyo
ni baada ya kuridhishwa na kiwango chake ndani
ya uwanja.

“Kocha mwenyewe leo (jana) amemuona akiwa
anacheza katika kikosi cha vijana cha U-20,
amevutiwa naye kutokana na uwezo mkubwa
aliokuwa anauonyesha, hivyo upo uwezekano
mkubwa wa kumsajili,” kilisema chanzo hicho.

Alipoulizwa Phiri kuhusiana na kiwango cha
James, alisema: “Ni mchezaji mzuri mwenye
uwezo mkubwa wa kucheza, ukiangalia anaweza
kukaba, kontroo yake nzuri na anapiga krosi
safi, kuhusu kumsajili siwezi kuzungumza hivi
sasa.”

0 comments:

Post a Comment