Msanii wa Marekani Shawn Carter, maarufu kama Jay Z, amenunua nembo ya Armand de Brignac ya kinywaji cha champagne. Kampuni ya mvinyo na vinywaji vikali ya New York, Sovereign Brands imesema imeuza nembo yake hiyo kwa Jay Z kwa kiasi ambacho hakikutajwa. Champagne hiyo, maarufu kama "Ace of Spades" au "Dume la Jembe" hutengenezwa na watu wanane tu katika mji wa Chigny-les-Roses nchini Ufaransa.
Mvinyo huo unaowekwa kwenye chupa ya dhahabu, ulitumika
na Jay Z katika video yake mwaka 2006. Chupa moja huuzwa kwa dola 300.
Ununuzi wa nembo hii unaingia katika orodha ndefu ya biashara za Jay Z,
nje ya muziki, ikiwemo kampuni ya kutengeneza nguo, mahoteli na 'label'
za kurekodi muziki. Jay anadhaniwa kuwa mwanamuziki wa hip-hop wa tatu
kwa utajiri duniani - utajiri wake ukikadiriwa kuwa takriban dola
milioni 520, kwa mujibu wa Forbes
0 comments:
Post a Comment