Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete
alifanyiwa upasuaji wa tezi dume
(prostrate) katika Hospitali ya Johns
Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la
Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais
Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya
madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya
yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji
matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja
unusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika
salama na kwa mafanikio makubwa.
Taarifa hiyo inasema hali ya Rais Kikwete
inaendelea vizuri japo bado yuko wodini
akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa
madaktari na kupatiwa tiba.
0 comments:
Post a Comment