Facebook

Tuesday, 11 November 2014

MISS TANZANIA MPYA NAYE UTATA MTUPU.....

 Photo: MISS TANZANIA 2014 sasa ni LILIAN KAMAZIMA
MISS Tanzania mpya wa 2014, Lilian
Kamazima, amesema alihisi ushindi tangu
alipoingia ka tika mashindano hayo, lakini
alipokosa taji hakuhuzunika bali alikubali
matokeo.
Lakini zengwe jipya limeibuliwa jana na
kuenezwa kwenye mitandao ya kijamii
kwamba Lilian aliyepewa taji hilo baada
ya Sitti Mtemvu ambaye ni mshindi wa
awali kujivua taji kutokana tuhuma za
kudanganya umri, si raia wa Tanzania
bali ni Mnyarwanda.
Hashim Lundenga ambaye ni Mkurugenzu
wa Miss Tanzania, amekanusha vilivyo na
kusisitiza kuwa ni uzushi kwa sababu
wao wanaangalia vyeti vya kuzaliwa
ambavyo vinaonyesha uraia wa mshiriki.
Hayo yameibuka siku mbili tangu Lilian
kukabidhiwa taji la Miss Tanzania 2014,
lililokuwa likishikiliwa na Sitti Mtemvu
aliyeamua kulivua baada ya kukumbwa
na kashfa mbalimbali tangu kutawazwa
kwake Oktoba 11.
Lilian ambaye awali alikamata nafasi ya
pili, alisema: “Sikuwa na kinyongo
ukizingatia urembo ni mambo mengi si
sura, ngozi, mwonekano pekee bali
unajumuisha mambo mengi, ndiyo maana
kipindi cha usahili huwa kirefu. Binafsi
niliamini kwamba (Sitti) alistahili hasa
kutokana na kuwa na vigezo vingi
vinavyoonekana kwa macho hata
tulipokuwa kambini, nilikubali matokeo,”
alisema Lilian.
Lilian alisema kipindi cha mwezi mmoja
tangu kutolewa kwa matokeo Oktoba 11,
anaamini kilikuwa kigumu kwa Sitti, pia
kwake hasa ukizingatia tuhuma
mbalimbali zilizokuwa zikimkabili
mrembo huyo aliyetokea katika Kanda ya
Temeke.
“Nina maono ya mbali na ninatamani
miaka mitano ijayo niione Tanzania
iliyokua hasa katika nyanja ya elimu,
napenda kuona namba ya wanafunzi
wanaofaulu ikiwa sawa vijijini na mijini
ili kuwa na taifa lenye watu werevu na
wenye maendeleo, hivyo nitajitahidi
kutumia nafasi yangu kusongesha
gurudumu hili,” alisema.
Mrembo huyo ambaye kwa sasa yupo
nchini Uganda kwa shughuli za masuala
ya mitindo, alisema anafurahia kupata
nafasi hiyo na anawaahidi Watanzania
kuwa atafanya kazi kwa nguvu zote ili
kuhakikisha anatimiza malengo ya
waandaaji wa mashindano hayo. Lilian
Kamazima ana miaka 18, alishiriki
akitokea Mkoa wa Arusha.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment