Wakazi katika mji mmoja nchini Taiwan wameahidiwa zawadi nono kwa kukamata mbu. Shindano hilo lilitangazwa na idara ya afya ya jiji la Kaohsiung, linalenga kupambana na mlipuko wa mbu wanaosababisha homa ya dengue katika eneo hilo.
Wakazi
wanatakiwa kukamata mbu wengi iwezekanavyo, wakiwa wazima au hata kama
wamekufa, na mtu atakayekamata mbu wengi zaidi atapewa zawadi ya dola
100, imesema idara ya afya. Mshindi wa pili na wa tatu watapewa dawa ya
kuzuia mbu na chandarua. Watu wanatakiwa kuwatega mbu hao, au kuhifadhi
'mizoga' yao, kwa sababu itawasilishwa mbele ya maafisa kwa ajili ya
kuhesabiwa.
"Badala ya kuwapiga faini watu wanaoshindwa kuweka mazingira
safi, tunadhani mradi huu utasaidia kuhamasisha ushirikiano," amesema
Ho Hui-ping, akizungumza na tovuti ya Focus Taiwan. Zaidi ya maambukizi
7,000 yameripotiwa mjini Kaohsuing, huku wagonjwa wapya mia mbili
wakipatikana kila siku, limeripoti gazeti la China Post.
0 comments:
Post a Comment