Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday, 28 February 2015

Henry aitaman kazi ya Arsene Wenger


Mchezaji mkongwe wa Arsenal Thierry Henry amefichua kuwa ndoto yake kuu ni kumrithi Mkufunzi Arsene Wenger katika kilabu ya Arsenal.
Mchezaji huyo wa zamani ambaye ndio anayeongoza kwa idadi ya mabao katika kilabu hiyo akiwa na magoli 228 aliripotiwa kupewa fursa ya kuanza kufunza soka katika chuo cha ukufunzi wa soka katika kilabu hiyo mapema mwezi huu.
Raia huyo wa Ufaransa amekiri kwamba ana mipango ya kumrithi Wenger wakati kocha huyo atakapoamua kustaafu.
Akizungumza wakati wa maonyesho ya Jonathan Ross Show,Henry alisema:

''Sijui ni kwa mda gani Wenger anataka kusalia kama mkufunzi wa Arsenal.
Lakini ni sharti niwe na uzoefu wa kutosha kuchukua wadhfa huo.
Kuwa Mkufunzi wa Arsenal ni ndoto yangu kubwa ,lakini nafaa kujifunza mwanzo ,hicho ndicho kitu muhimu''.

UTAFITI:Wanaolala sana kuugua kiharusi


Watu wanaolala kwa zaidi ya masaa manane kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kiharusi,utafiti umesema lakini wataalam hawajua sababu yake.
Utafiti uliofanywa kwa takriban watu 10,000 katika chuo kikuu cha Cambridge ulibaini kwamba wale wanaolala kwa takriban saa nane wana uwezekano mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi.
Watu wazima hupendelea kulala kati ya saa sita na tisa ili kupumzika vizuri,lakini kulala zaidi hushirikishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa sukari pamoja na ule wa kunenepa kupitia kiasi.
Hatahivyo haijabainika kutoka kwa utafiti huo iwapo kulala kwa zaidi ya saa nane huenda ndiko kunakosababisha matatizo hayo ambayo husababisha kiharusi ama iwapo ni miongoni mwa sababu za magonjwa yasiojulikana.
Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu walioko na kati ya miaka 42 na 81.
 
Watafiti walichunguza mienendo yao ya kulala kwa kipindi cha miaka 10 ambapo watu 346 walipatwa na kiharusi.
Baada ya kuangazia athari kama vile miaka na jinsia, watu waliosema wamekuwa wakilala kwa zaidi ya masaa manane walipatikana na hatari ya asilimia 46 kupatwa na ugonjwa huo.
Wale walioweza kulala kwa chini ya masaa sita walipatikana na hatari ya asilimia 18

Di Maria ajuta kujiunga na Man United


Mchezaji nyota ambaye pia ni kiungo wa kati wa Manchester United Angel Di Maria amesema kuwa alifanya makosa kujiunga na Kilabu ya Manchester United msimu uliopita.
Raia huyo wa Argentina amejaribu kuendana na maisha ya ligi ya Uingereza na majuto yake yataongeza uvumi kwamba anapanga kuondoka katika kilabi hiyo miwshoni mwa msimu huu.

Mwandishi wa Uhispania Manolete Esteban anadai kwamba mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Real Madrid ambaye amekosolewa kwa uchezaji wake amewaambia marafiki zake kwamba anajuta kuondoka katika kilabu ya Real Madrid.
Esteban aliiambia runinga ya Uhispania katika kipindi cha La Goleada kwamba Di maria alikiri kwa rafikiye katika kilabu ya Real Madrid kuwa anajuta kujiunga na Manchester United.

SOURCE:BBC SPORTS

UCHAMBUZI MECHI ZA LEO J'MOSI LIGI KUU UINGEREZA n HISPANIA NA Mr.CHOI {KWA TAARIFA YAKO}

 
__________________________________________________

MANCHESTER UNITED vs SUNDERLAND 18:00
                

   Kama unakumbuka msimu uliopita katika mchezo kama huu uliyo fanyika Old Trafford tulishuhudia Man Utd wakifungwa 1-0 kwa goli la Larsson dakika ya 30.
   Baada ya kufungwa na Swansea na kupelekea wengi kuhoji uwezo wa Van Gaal katika kuifundisha Man Utd licha ya CV nzuri alizokuwa nazo pengine huu ni miongoni mwa michezo itakayo kuwa migumu mbele yake kulingana na matokeo yasio mazuri ya wapinzani wake hivi karibuni walio chini ya Poyet.
   Man Utd imekuwa haichezi kama timu shindani katika kuwania nafasi muhimu licha ya kuwa na kikosi bora kabisa hata pale. 

Wengi tulipajua kama machinjioni hivi sasa mambo yamebadilika.
   Wanakutana na Sunderland timu isiyo eleweka katika kila mchezo na licha ya kuwakosa Billy Jones,Rodwell na Will Buclley bado safu yao ya ushambuliaji ni nzuri hasa ikichagizwa na kasi ya Johnson,Defoe, Fletcher ambao mabeki wa Man Utd wasipo kuwa makini hasa kukatika ovyo itawagharimu.

   Licha ya majeruhi ya Van Persie, Carrick lakini ukubwa wa kikosi chao haitokuwa pengo kwa mchezo kama huu kutokana na uwepo wa wachezaji walio na uwezo kuziba mapengo yao.
  

Katika michezo mitano iliyopita Man-utd kashinda 3,D-1,L-1 huku wapinzani wao wakishinda mara 1,D-2,L-2.

NB:: Katika michezo 13 ya hivi karibuni pale Old Trafford, Man Utd wameshinda michezo 10,wametoa sare michezo 2 na kupoteza 1.
   - Sunderland wametoa sare michezo mingi zaidi 13 katika michezo 26 zaidi ya timu nyingine katika historia ya ligi.


_________________________________________________________________________________
 
WEST HAM vs CRYSTAL PALACE 15:45               
 Leo katika "London derby" nyingine pale Upton park tutashuhudia "British football" kati ya Big Sam na Allan Pardew.
   Baada ya kutoa sare katika "derby" dhidi ya Spurs huku katika michezo mitano iliyopita akifungwa miwili na kutoa sare mitatu bado bado kikosi cha Big Sam ni miongoni mwa vikosi vyenye ushindani katika kila mechi licha ya kuwa na majeruhi kadhaa.
   Sakho akiwa mfungaji bora wa timu hiyo kwa jumla ya magoli 9 huku akitengeneza ushirikiano mzuri na Valencia watakuwa sumu mbele ya safu ya ulinzi ya Crystal Palace huku pia Nene akirejea baada ya majeruhi na Amalfitano akiendelea na adhabu ya kukosa michezo 3 na huu ni mchezo wa 2.
   Vijana wa Pardew watawakosa Sanogo,Camplell,Lee na Chamakh walio majeruhi lakini Jedinak muuaji ambaye msimu uliopita alifunga goli la ushindi (1-0) dhidi ya W.ham hapo Upton bado haija julikana na Mcarther, katika michezo  mitano iliyopita Pardew kashinda 1,D-1,L-3.
  Tutaraji mchezo wa kibabe kwa pande zote hasa katika safu ya kiungo kwani timu zote zinaviungo wenye nguvu, Song-noble, Gayle-Jedinak kama akicheza.

NB:: W.ham imepoteza mchezo 1 kati ya 11 ya hivi karibuni katika uwanja wake wa nyumbani.
-------------------------------------------------------------------------------
  
WEST BROM vs SOUTHAMPTON   18:00
Pale The Hawthorns, West Brom walio katika ubora hivi sasa baada ya Tony Pulis kujiunga takribani mwezi mmoja huku katika michezo 6 akipoteza 1 na kufudhu robo fainal ya FA watacheza dhidi ya Southampton walio katika kinyang'anyiro cha kucheza Uefa mwakani.
   Watamkosa Morrison huku Anichebe akirejea wakati Soton wataendelea mkosa Toby,J.Rodriguez
   Tutaraji mchezo mgumu sana kutokana na aina ya uchezaji kwa pande zote,Soton wanacheza kwa spidi sana huku wenyeji wao maranyingi wanalinda goli na kufanya mashambulizi ya kustukiza pia katika michezo 3 iliyopita W.brom hawajafunga goli mbele ya Soton.


NB::West Brom imefunga magoli mengi 8 kutokana na kona zaidi ya timu zote katika ligi ukiwaondoa Chelsea walio sawa .
  -Katika michezo 7 ni mchezo mmoja tu ndo golikipa Foster karuhusu goli chini ya T.Pulis.
_______________________________________________________

GRANADA vs BARCELONA 18:00                 
  Los Carmenes uwanja wa nyumbani wa Granada walio chini ya Abel Resino watakwaana na wababe wa Man City,Fc Barcelona.
   Katika mchezo uliofanyika Camp Nou tulishuhudia Barcelona wakishinda 6-0 huku Neymar akifunga magoli matatu vijana hawa wa Resino watamkosa mshambuliaji wao tegemezi Youssuf-El Arabi huku Colunga akiwa majeruhi.

   Barcelona wao watamkosa Pique baada ya kufungiwa huku Mathieu akitarajiwa chukua nafasi ya mkongwe huyo.
   Baada ya kufungwa na Malaga goli la mapema kabisa na kusimamisha ushindi wa michezo 11 mfululizo katika mashindano mbalimbali  kinaweza kuwapa kujiamini kwa Granada kufanya vyema katika mchezo huu ambao Barca wakipoteza itawapa fursa Real kutanua wigo wa pointi dhidi yao.


    MSN kombinenga baada ya kufanya vyema Uefa watataraji endeleza moto walio uwasha tangu mwaka uanze huku Messi akitafuta goli 3 kumfikia Cristian Ronaldo..
  Ngoja tusubiri kama Granada walio nafasi ya 19 watashinda ilikujinasua na kushuka daraja kingine tutaraji kujilinda zaidi kwa Granada na mashambulizi ya kustukiza dhidi ya Barca walio nafasi ya 2.


NB:: Katika michezo 7 iliyopita Granada wameshinda mchezo 1 dhidi ya Barca.

_______________________________________________________


Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa uchambuzi makini katika masuala mbalimbali hususan michezo.

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

 Imeandaliwa na................
                                                Mr CHOI
                                             Choikangta.ckt@gmail.com
                                               WhatsApp -0765 691418

Ben Pol:Kiukweli Wanigeria Hawatuwezi Kimuziki



Msanii Ben Pol ambae kwa sasa anafanya poa na kazi yake mpya ya Sophia amefunguka na kusema kuwa wasanii wa Nigeria hawawawezi wasanii wa bongo kwa kipaji na kutengeneza ngoma kali na hilo amelithibitisha msanii Diamond Platnum ambae kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa Nitampata wapi ambao unaoneka kufanya vizuri zaidi kuliko hata ngoma za wasanii wa Nigeria katika baadhi ya vituo vya habari ndani na nje ya Tanzania.

Ben Pol amesema hayo kupitia Account yake ya Twitter ambapo amesema msanii Diamond kishamfunga paka kengele na kilichobaki ni kuongeza nguvu na kuona ni jinsi gani wanaweza kupenya zaidi na kuzidi kutanua mipaka ya Bongo fleva ulimwenguni.


"Kiukweli Wanigeria Hawatuwezi Kimuziki,Na kuhusu Nani Atamfunga Paka kengele, Tayari Diamond Ameshamfunga Paka kengele"
Ben Pol amekuwa msaniii wa pili kuonyesha kuwa muziki wa Bongo fleva ni muziki mzuri kuliko muziki wa Nigeria kwani hata msanii Mwanafalsafa alishasema kuwa haupendi na haukubali kabisaa muziki wa Nigeria.Licha ya baadhi ya wasanii kuusujudu na kuamini ndiyo muziki mzuri na ambao wanahisi unapendwa sana kwa sasa lakini kwa Mwana Fa imekuwa tofauti kwani alisema "Katika Habari nyingine,nimeamua kuwa hater wa mziki wa Nigeria".

Kwa upande wake Diamond amezidi kushukuru Mungu kuona wimbo wake huo wa Nitampata wapi unazdi kuchana mawimbi na kupokelewa vizuri hata nje ya Afrika Mashariki kitu ambacho kinamfanya kujiona ni balozi mzuri zaidi wa Afrika Mashariki.
"Asante Sana Mwenyez Mungu kwa Baraka zako zinazonifanya nizidi kuiwakilisha vyema Nchi yangu na Afrika Mashariki yangu..."

BantuTz MAGAZETINI:-SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO FEBRUARI 28

.
BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa katika kurasa za mbele na nyuma magazeti yote ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC00018
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
 Endelea kufurahia huduma za BantuTz.com huku ukiusubiria kwa hamu Mtandao wa kijamii mkubwa na wa kisasa zaidi uitwao Bantuz mwaka huu

Vanessa Mdee na Jux wadhihirisha mahaba mazito wakiwa Afrika Kusini

Vanessa Mdee na Jux wote wapo nchini Afrika Kusini walikoenda kufanya video ambayo hata hivyo hawajasema ni ya wimbo gani na kwa mujibu wa picha wanazopost kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wanapeana kampani ya nguvu.
Hawajawahi kukubali hadharani kuwa ni wapenzi lakini picha zinaonesha wazi kuwa mastaa hao wapo kwenye dimbwi zito la mapenzi.

Kupromote wimbo wake mpya ‘Nikuite Nani’, Jux amepost picha akiwa na hitmaker huyo wa ‘Hawajui’ anayeonekana ‘akimchumu’ kwenye paji la uso.

Kabla ya picha hiyo, Jux alipost nyingine kadhaa akiwa na mrembo huyo katika pozi ambalo huwezi kuuliza kama ni marafiki tu.!

Hivi karibuni Vanessa Mdee aliiambia BantuTz kuhusu uhusiano wake na Jux: I actually I like to keep my private life private. Nadhani kuna baadhi ya mambo ambayo hayahitaji majibu.”

Jux na Vanessa wameongozana na Weusi na Navy Kenzo kwenye safari hiyo ya South.

Daktari wa Rais wa Rwanda auawa baada ya kupigwa risasi na Polisi Kigali-Rwanda.

 Polisi wamempiga risasi na kumuua daktari wa zamani wa Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati akiwa katika kituo cha Polisi, Kigali.
- Inasemekana akiwa na maaskari aliomba kwenda Msalani ambako aliruhusiwa, kisha aliporudi alitaka kupora silaha kwa askari, hivyo kusababisha kifo chake.
Another ”mysterious” death in Rwanda. WHO? Dr. Gasakure (Kagame’s personal doctor)

WHAT happened?
The Medical Doctor is said to have been in police custody for ” a series of crimes” including malicious destruction of property and illegal arrest and detention of some Rwandans!!!

HOW was he killed?

While in police custody Kagame’s personal doctor asked for, and was given, permission to go to the bathroom ( toilet). While going to the toilet, the Medical Doctor wanted to grab a gun from the police officer ( on duty in the toilet?). The police officer shot and killed Dr. Gasakure, RIP. That’s Kagame junta official narrative.

What isn’t the junta telling us?
Kagame suspects that there is a Tutsi inner circle conspiracy to assassinate him using poison or a bullet. It’s alleged that Dr. Gasakure ( and the Rwandan artist – Kizito – who is in prison was part of the ” poison” conspiracy!!! Every ” suspect” must be killed for the protection of the Hitler of Africa.

Question: How many people should Kagame kill before he’s stopped?

Mmiliki wa Blog auawa kinyama Bangladesh


Mwanablogu mmoja mwenye asili ya Marekani na ile ya Bangladeshi- maarufu kwa maoni ya kumkana Mungu ameuawa kinyama alipozuru mji wa Dhaka.
Avijit Roy - ambaye alikuwa akiishi Marekani - alikuwa amezuru mji huo mkuu wa Bangladeshi na mkewe kuhudhuria dhifa ya uzinduzi wa kitabu.
Alikuwa amepokea vitisho baada ya kuchapisha makala ya kupigia debe maoni huru, sayansi na maswala ya jamii, ambayo yamekuwa yakikosolewa na kutajwa kuwa ni kinyume cha dini ya Uislamu.
Polisi wanasema wanachunguza kuuwawa kwake lakini kufikia sasa hakuna aliyetiwa mbaroni.

Friday, 27 February 2015

Lupita Nyong'o aibiwa vazi lake la bei Mbaya


Nguo iliyobuniwa na kampuni ya Calvin Klein yenye thamani ya dola 150,000, na kuvaliwa na msanii maarufu wa kike Lupita Nyong'o katika tuzo za Oscar imeibiwa Hollywood .
Gauni hilo lililobuniwa kwa namna ya pekee na kupambwa kiasilia na konokono weupe zaidi ya 6,000 toka baharini, lilichukuliwa kwenye hoteliya London magharibi mwa Hollywood.

Lupita Nyong'o kutoka nchini Kenya aliibuka msanii bora wa kike mwaka jana baada ya miaka kumi na mbili ya utumwa, Lupita alikuwa mtangazaji wa sherehe za jumapili.
Baadhi ya magazeti yanamwita Lupita Nyong'o mrembo wa mwaka 2014.
Sheriff William Nash anasema nguo hiyo inaonekana kuibiwa siku ya jumatano jioni na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kupitia kamera maalum za CCTV.

Mwanaume ajitokea bikra siku ya wanawake duniani.

Mwanamume mmoja amejitolea kutoa ubikira wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake.
Sorin Gorgian Salinievcici mwenye umri wa miaka 24 amejitolea kuuza ubikira wake kwa pauni 1,476 baada ya kusoma kuhusu wanawake wanaofanya hivyo.
Alielezea kuwa :''mimi husoma kuhusu wasichana wanaofanya hivyo na nikafikiri kwamba iwapo wanafanya hivyo hata mimi naweza kufanya''.

Amesema kuwa mwanamke yeyote atakayenunua ubikira wake ni sharti awe mwenye heshima.
''Sisemi kuwa ni lazima awe mrembo lakini awe mwanamke wa kawaida, mzuri na mwaminifu''.alisema.
Katika bango aliloandika nyumbani kwake huko Romania,alisema kuwa inaweza kuwa zawadi nzuri katika maadhimisho ya siku hiyo ya wanawake mnamo mwezi machi tarehe 8.

Je,unadhani kitendo hiki kinakubalika?

MAAJABU:Upandikishaji wa kichwa sasa unawezekana

Unaposikia habari hii utadhani ni maudhui ya filamu ya kutisha ,lakini wanasayansi wanaamini upasuaji wa upandikishaji wa kichwa cha mwanadamu katika mwili mwengine huenda ukafanikiwa.
Madaktari watazindua mradi huo katika kongamano wakati wa msimu wa joto ,kwa lengo la kuanzisha utaratibu huo mnamo mwaka 2017.

Mtu atakayeongoza mpango huo ni daktari raia wa Italy Sergio Canavero kutoka kundi moja la wanasayansi mjini Turin.

Anaamini kwamba upandikishaji wa vichwa vya watu utawasaidia wanaosumbuliwa na magonjwa ya misuli na saratani.
Baada ya kutoa wazo hilo mnamo mwaka 2013,daktari Canavero anaamini vikwazo vikuu vya upasuaji huo vimekabiliwa ,kulingana na ripoti mpya ya wanasayansi.

Vikwazo hivyo ni pamoja na usimamizi wa uti wa mgongo kuingiliana na kichwa kipya pamoja na kuhakikisha kuwa kinga ya mwili haikikatai kiungo hicho kipya.
Daktari Canevaro alichapisha taarifa iliokuwa na nadharia kuhusu vile anavyoamini upasuaji huo unaweza kufanyika

Watu 17 wauawa kwa Bomu nchini Nigeria



Takriban watu 17 wameuawa kwa Bomu la kujitoa muhanga katika kituo cha mabasi mjini Biu, huku mtu mwingine aliyekuwa na nia ya kujitoa muhanga ameripotiwa kukamatwa na Watu na kupigwa mpaka mauti yakamkuta.
Mjini Jos, Watu 15 waliuawa kwa mabomu matatu yaliyorushwa kutoka kwenye Gari katia eneo la kituo cha mabasi na Chuo kikuu.
Uchaguzi wa Urais mwezi Februari umeahirishwa kwa sababu ya machafuko.
Uchaguzi sasa unatarajiwa kufanyika tarehe 28 mwezi March

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ambaye alikuwa na ziara kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, mjini Baga, amesisitiza kuwa Jeshi linawakabili wanamgambo wa Boko Haram.
Jeshi lilirudisha mji wa Baga kutoka mikononi mwa Boko Haram Wiki iliyopita .Kundi hilo bado linakabili sehemu kubwa ya Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Borno na zaidi ya Watu milioni tatu wamekimbia makazi yao.
Mashambulizi mjini Kano na Potiskum siku ya jumanne yaligharimu maisha ya Watu zaidi ya 50.Hakuna kundi lolote lililokiri kutekeleza mashambulizi hayo

Ndege ya Jeshi yaanguka na kuwaka moto uwanja wa ndege Mwanza, rubani anusurika!

Taarifa kutoka Mwanza Airport ni kuwa kuna ndege ya Jeshi imelipuka na kuteketea.

Rubani wa ndege hii, ndg Peter Augustino kafanikiwa kuruka kwa parachuti na kunusurika ingawa inadaiwa kavunjika mguu na kukimbizwa hospitali.




Dkt. Magufuli aongoza wananchi kwenye majaribio ya uzinduzi wa kivuko cha MV Dar es Salaam


Leo Dkt.Magufuli amewaongoza wananchi wa Dsm kwenye majaribio ya uzinduzi wa Kivuko kipya Cha MV DAR ES SALAAM kitakachofanya safari zake kati ya Dsm na Bagamoyo, ambapo mamia ya wananchi walkiwana Waziri Magufuli wamesafiri bure kutoka Dsm kwenda Bagamoyo na kurudi.

AVEVA: Sina mpango wa kujiuzulu Simba.

Dar es Salaam. Wakati kuna madai ya mpasuko wa uongozi, ukata mkubwa na madeni kwenye klabu ya Simba, rais wa klabu hiyo Evance Aveva amesema ajiuzulu, wanaotaka afanye hivyo wafuate taratibu. Akizungumza na gazeti hili jana, Aveva alisema kuwa kuna vyombo rasmi ambavyo vinafanya kazi ndani ya klabu hiyo zikiwamo kamati za kisheria, kamati ya mashindano, kamati ya utendaji na kwamba kama kuna tatizo wanachama wanajua taratibu za kufuata.
"Matokeo ya mpira ni hali ya mchezo, tumewapa wachezaji kila kitu, hakuna mchezaji anayedai zaidi ya posho yao ya muda ya mchezo wao na JKT Ruvu, Sh600,000 na kule Shinyanga viongozi wote tulikwenda na kuna motisha walipewa, sasa kosa letu viongozi ni lipi?"alihoji

"Mkutano mkuu wa wanachama upo pale pale, utafanyika Machi Mosi, wanachama walio hai wajitokeze kwa wingi pale Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam,"alisema.
Alieleza kuwa hakuna tofauti kati yake namakamu wake, Geoffrey Nyange 'Kaburu' ambaye inadaiwa kamati ya utendaji ya klabu hiyo imempiga marufuku kujihusisha na masuala ya timu.
Kumekuwa na madai kuwa Kaburu amezuiwa kwa kile kwa kuwa amekuwa akimwingilia kocha (Goran) majukumu yake ikiwa ni pamoja na kugawa wachezaji.

"Madai hayo Kaburu tulimuuliza akakataa, hatuna ugomvi wowote naye, ni kiongozi mwenzetu na tunaelewana vizuri na muda si mrefu nimetoka kuzungumza naye kwa simu, alichaguliwa na wanachama kama mimi, hatujafikia hatua ya kusimamishana, viongozi wote tupo kitu kimoja,"alisema.
Kwa upande wake, Kaburu hakupatikana jana kuzungumzia mgogoro wake na viongozi wenzake licha ya kutafutwa kwa muda mrefu.

CHANZO:MWANANCHI