Facebook

Friday, 27 February 2015

AVEVA: Sina mpango wa kujiuzulu Simba.

Dar es Salaam. Wakati kuna madai ya mpasuko wa uongozi, ukata mkubwa na madeni kwenye klabu ya Simba, rais wa klabu hiyo Evance Aveva amesema ajiuzulu, wanaotaka afanye hivyo wafuate taratibu. Akizungumza na gazeti hili jana, Aveva alisema kuwa kuna vyombo rasmi ambavyo vinafanya kazi ndani ya klabu hiyo zikiwamo kamati za kisheria, kamati ya mashindano, kamati ya utendaji na kwamba kama kuna tatizo wanachama wanajua taratibu za kufuata.
"Matokeo ya mpira ni hali ya mchezo, tumewapa wachezaji kila kitu, hakuna mchezaji anayedai zaidi ya posho yao ya muda ya mchezo wao na JKT Ruvu, Sh600,000 na kule Shinyanga viongozi wote tulikwenda na kuna motisha walipewa, sasa kosa letu viongozi ni lipi?"alihoji

"Mkutano mkuu wa wanachama upo pale pale, utafanyika Machi Mosi, wanachama walio hai wajitokeze kwa wingi pale Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam,"alisema.
Alieleza kuwa hakuna tofauti kati yake namakamu wake, Geoffrey Nyange 'Kaburu' ambaye inadaiwa kamati ya utendaji ya klabu hiyo imempiga marufuku kujihusisha na masuala ya timu.
Kumekuwa na madai kuwa Kaburu amezuiwa kwa kile kwa kuwa amekuwa akimwingilia kocha (Goran) majukumu yake ikiwa ni pamoja na kugawa wachezaji.

"Madai hayo Kaburu tulimuuliza akakataa, hatuna ugomvi wowote naye, ni kiongozi mwenzetu na tunaelewana vizuri na muda si mrefu nimetoka kuzungumza naye kwa simu, alichaguliwa na wanachama kama mimi, hatujafikia hatua ya kusimamishana, viongozi wote tupo kitu kimoja,"alisema.
Kwa upande wake, Kaburu hakupatikana jana kuzungumzia mgogoro wake na viongozi wenzake licha ya kutafutwa kwa muda mrefu.

CHANZO:MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment