Siku chache baada ya kuzinduliwa kwa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 na Rais Jakaya Kikwete, chama cha NCCR Mageuzi kimesema sera hiyo haina manufaa yenye tija kwa wananchi.
iku chache baada ya kuzinduliwa kwa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 na Rais Jakaya Kikwete, chama cha NCCR Mageuzi
kimesema sera hiyo haina manufaa yenye tija kwa wananchi bali sera hiyo
imelenga uchaguzi mkuu kwa kuwalaghai wapiga kura na sio kutekeleza yaliyomo ndani ya sera hiyo.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi taifa Mh James Francis Mbatia ameyabainisha hayo mbele ya waandishi wa habari jijini.
Dar es Salaam wakati akieleza masuala mbalimbali yaliyoanishwa ndani ya sera mpya ya elimu ambayo imeandaliwa kwa muda wa miaka saba hadi kukamilika kwake na kuzinduliwa Februari 13 mwaka huu na Rais Jakaya
Kikwete na kuanisha mpango wa serikali wa kutoa elimu bure pindi sera
hiyo itakapoanza kutumika jambo ambalo amelieza kuwa ni kutendawili
kisichokuwa na jibu kamwe.
Kuhusu muda
wa kipindi cha miaka saba kilichotumika kuiandaa sera hiyo hadi
kukamilika kwake Mh Mbatia amesema ni muda mrefu umetumika huku sera
ikiwa imegubikwa na makosa mengi ya uchapaji pamoja na kushindwa kwenda
na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya sasa duniani hivyo sera
imeshapitwa na wakati hata kabla haijaanza utekelezaji wake kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment