Kampuni ya Sony imetangaza wiki hii kwamba itajiondoa katika michezo ya kielektroniki katika idara zake za sauti na video.Badala yake inapanga kuangazia maeneo matatu ikiwemo idara yake ya filamu,burudani,michezo yake ya Playstation mbali na kuuza picha kwa kampuni za Apple na Iphone.
Hatahivyo habari hiyo haijaizuia kampuni
hiyo kuonyesha mipango yake ya vazi lake la machoni.Kampuni hiyo ya
teknologia kutoka japan inachukua maagizo ya mapema ya miwani yake aina Smarteyeglass,ambayo itafanya kazi kwa ushirikiano wa vifaa vyenye programu ya Android ili kuonyesha picha katika vioo vya miwani hiyo.Lakini ikiwa na uzito wa gramu 77ni mizito sana,mipana na mizuri ikilinganishwa na miwani ya Google.
0 comments:
Post a Comment