SOUTHAMPTON vs LIVERPOOL 19:15
Baada ya kuondoka kwa kocha Mauricio Pochettino na kutimkia
Tottenham kisha kuuzwa kwa R.Lambert, Adam Lallana, Dejan Lovren na Shaw
wengi walitaraji kuiona Soton ikiwa miongoni mwa timu zitakazo fanya
vibaya msimu huu.
Lakini pia hata msimu ulivyo anza na vijana hawa wa Koeman kufanya
vyema bado maneno yakasikika ni nguvu za soda na watawaachia wenye
nafasi zao ila mpaka sasa mambo ni tofauti kwani mpaka sasa kuna
asilimia kubwa kwa wao kucheza michuano ya Uefa.
Itakuwa pale St Mary’s Stadium ambapo wata pambana na Liverpool huku
chagizo la mchezo ni urejeo wa Lalana ,Lambert pale St Mary's lakini pia
baada ya jana Man United kupoteza dhidi ya Swansea itakuwa nafasi kwao
kufanya vyema na kuwatoa Arsenal nafasi ya tatu.
Morgan Schneiderlin Matt Targett na Shane Long watarejea baada ya
majeraha lakini watawakosa Toby Alderweireld, Jay Rodriguez, Emmanuel
Mayuka na Ryan Bertrand, ngoja tusubiri kina Mane mbele ya Škrtel.
Liverpool walio nafasi ya saba kwa pointi 42 ambao wanatafuta nafasi
ya kuwa nne za juu hivi sasa wanacheza vyema huku wakichagizwa na uwepo wa
Sturridge pia Raheem Sterling anaweza anza katika mchezo kumbuka amekuwa
na mchezo mzuri pindi akikutana na Soton Gerrard hatokuwepo kutokana na
majeraha lakini safu nzima ya ushambuliaji iko fiti dhidi ya Soton
Michezo mitano iliyopita kwa timu zote Soton,W-2,L-2,D-1 kwa upande wa Liver,W-4,D-1.
NB:: The Reds mpaka sasa wamefunga penati 101 katika ligi kuu zaidi ya timu nyingine yoyote.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
TOTTENHAM vs WEST HAM 15:00
Pale katika dimba la White Hart Lane vijana wa Mauricio
Pochettino watapambana na vijana wa Big Sam mzee wa kutafuna kiboko ya
timu kubwa.
Mshambuliaji hatari Kane, Ryan Mason and Mousa Dembele wanataraji
kuanza hii leo baada ya kupumzishwa katika mchezo wa Europa ligi dhidi
ya Fiorentina walitoka sare ya 1-1.
Pasipo kuwa na majeruhi Spurs walio nafasi ya 6 na pointi 43
watahitaji kushinda ilikupata matumaini ya kucheza Uefa huku katika
michezo mitani iliyopita wameshinda mara-2,D-2,L-1.
Bilashaka mshambuliaji KANE ambaye katika michezo 10 amefanikiwa
kufunga goli 11 atakuwa ni mwiba kwa safu ya ulinzi ya West Ham.
Kwa upande wa West Ham watachagizwa na urejeo wa Winston Reid na James
Collins huku wakiwa nafasi ya 8 point 38 katika michezo mitano
wakishinda mchezo 1,D-2,L-2.
Kikubwa Big Sam anatafuta nafasi ya kucheza Europa hivyo siku ya leo
atahitaji ushindi ilikusogeza ndoto zake, Morgan Amalfitano amefungiwa
hatokuwepo huku wakimkosa Andy Carroll msimu wote uliobakia.
Tutaraji mchezo wa ushindani sana kutokana na uchezaji wa timu zote
hasa W.ham ambao wamekuwa na kila mbinu ndani ya uwanja katika michezo
miwili iliyopita ya timu hizi kulikuwa na kadi nyekundu tatu.
Spurs ndo timu iliyo ruhusu penati nyingi mpaka sasa katika ligi
penati 7 huku West Ham ndiyo timu iliyofunga magoli mengi ya kichwa 14 mpaka
sasa.
NB::
Tottenham imepitisha kuanza kujenga Uwanja mpya wa White Hart Lane
ambao utagharimu kitita cha pauni milioni 400.Uwanja huo utakuwa na
uwezo wa kuchukua watazamani 56,000 walioketi. Unatarajiwa kuwa
umekamilika na kuanza kutumika katika msimu wa 2018-19.
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
ELCHE vs REAL MADRID
Vijana wa kitongoji cha ,Elche katika jiji la Valencia wanao
ongozwa na Fran Escribá watakuwa katika uwanja wa nyumbani pale Martínez
Valero kuwakabiri Real Madrid.
Elche ambayo ipo nafasi ya 17 wakiwa na pointi 23 wataingia katika
mchezo huu kwa kumbukumbu ya kufungwa 5-1 katika mchezo uliofanyika
S.Bernabeu huku pia ikiwa ni miongoni mwa timu zenye safu mbovu ya
ulinzi inayo ongozwa na Tyton; Albacar, Lomban, Roco, Suarez wakiwa
wameruhusu goli 42 mpaka sasa.
Safu ya ushambuliaji inayo ongozwa na Mbrazil Jonathas mwenye goli 9
ndo jicho kwa vijana hawa wa Escribá huku mchezaji anaye fuata kwa
wingi wa magoli ni kiungo Victor mwenye goli 3. Katika michezo mitano
iliyopita wameshinda 3 na kupoteza michezo 2 .
Vinara wa La-Liga Real Madrid wenye pointi 57 watahitaji kushinda
mchezo huu ilikufikisha pointi 60 na kuwaacha Barca waliopoteza jana kwa
tofauti ya pointi 4.
Bado watawakosa Fabio Coentrao,Sami Khedira,James Rodriguez,Sergio
Ramos na Luka Modriç. Lakini wacheza kama Silva ,Illarramendi,Isco na
wengineo watajaza nafasi kama ilivyo kuwa katika mchezo wa Uefa dhidi ya
Schalke-04.
Katika michezo 5 Real Madrid wameshinda michezo 4 na kupoteza 1 ambao ulikuwa ule wa A.madrid.
BBC ambayo tangu mwaka uanze haijafanya vyema mbele ya MSN ya Barca
pengine kutokana na ubovu wa safu ya ulinzi ya Elche wanaweza fanya
vyema leo huku Cristian Ronaldo akihitaji kuongeza utofauti wa idadi ya magoli dhidi ya Messi
kwani anagoli 28 na mpinzani wake anagoli 26.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa uchambuzi makini katika masuala mbalimbali hususan michezo.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Imeandaliwa na................
CHOIKANGA
Choikangta.ckt@gmail.com
WhatsApp -0765 691418
0 comments:
Post a Comment