Facebook

Saturday, 28 February 2015

UCHAMBUZI MECHI ZA LEO J'MOSI LIGI KUU UINGEREZA n HISPANIA NA Mr.CHOI {KWA TAARIFA YAKO}

 
__________________________________________________

MANCHESTER UNITED vs SUNDERLAND 18:00
                

   Kama unakumbuka msimu uliopita katika mchezo kama huu uliyo fanyika Old Trafford tulishuhudia Man Utd wakifungwa 1-0 kwa goli la Larsson dakika ya 30.
   Baada ya kufungwa na Swansea na kupelekea wengi kuhoji uwezo wa Van Gaal katika kuifundisha Man Utd licha ya CV nzuri alizokuwa nazo pengine huu ni miongoni mwa michezo itakayo kuwa migumu mbele yake kulingana na matokeo yasio mazuri ya wapinzani wake hivi karibuni walio chini ya Poyet.
   Man Utd imekuwa haichezi kama timu shindani katika kuwania nafasi muhimu licha ya kuwa na kikosi bora kabisa hata pale. 

Wengi tulipajua kama machinjioni hivi sasa mambo yamebadilika.
   Wanakutana na Sunderland timu isiyo eleweka katika kila mchezo na licha ya kuwakosa Billy Jones,Rodwell na Will Buclley bado safu yao ya ushambuliaji ni nzuri hasa ikichagizwa na kasi ya Johnson,Defoe, Fletcher ambao mabeki wa Man Utd wasipo kuwa makini hasa kukatika ovyo itawagharimu.

   Licha ya majeruhi ya Van Persie, Carrick lakini ukubwa wa kikosi chao haitokuwa pengo kwa mchezo kama huu kutokana na uwepo wa wachezaji walio na uwezo kuziba mapengo yao.
  

Katika michezo mitano iliyopita Man-utd kashinda 3,D-1,L-1 huku wapinzani wao wakishinda mara 1,D-2,L-2.

NB:: Katika michezo 13 ya hivi karibuni pale Old Trafford, Man Utd wameshinda michezo 10,wametoa sare michezo 2 na kupoteza 1.
   - Sunderland wametoa sare michezo mingi zaidi 13 katika michezo 26 zaidi ya timu nyingine katika historia ya ligi.


_________________________________________________________________________________
 
WEST HAM vs CRYSTAL PALACE 15:45               
 Leo katika "London derby" nyingine pale Upton park tutashuhudia "British football" kati ya Big Sam na Allan Pardew.
   Baada ya kutoa sare katika "derby" dhidi ya Spurs huku katika michezo mitano iliyopita akifungwa miwili na kutoa sare mitatu bado bado kikosi cha Big Sam ni miongoni mwa vikosi vyenye ushindani katika kila mechi licha ya kuwa na majeruhi kadhaa.
   Sakho akiwa mfungaji bora wa timu hiyo kwa jumla ya magoli 9 huku akitengeneza ushirikiano mzuri na Valencia watakuwa sumu mbele ya safu ya ulinzi ya Crystal Palace huku pia Nene akirejea baada ya majeruhi na Amalfitano akiendelea na adhabu ya kukosa michezo 3 na huu ni mchezo wa 2.
   Vijana wa Pardew watawakosa Sanogo,Camplell,Lee na Chamakh walio majeruhi lakini Jedinak muuaji ambaye msimu uliopita alifunga goli la ushindi (1-0) dhidi ya W.ham hapo Upton bado haija julikana na Mcarther, katika michezo  mitano iliyopita Pardew kashinda 1,D-1,L-3.
  Tutaraji mchezo wa kibabe kwa pande zote hasa katika safu ya kiungo kwani timu zote zinaviungo wenye nguvu, Song-noble, Gayle-Jedinak kama akicheza.

NB:: W.ham imepoteza mchezo 1 kati ya 11 ya hivi karibuni katika uwanja wake wa nyumbani.
-------------------------------------------------------------------------------
  
WEST BROM vs SOUTHAMPTON   18:00
Pale The Hawthorns, West Brom walio katika ubora hivi sasa baada ya Tony Pulis kujiunga takribani mwezi mmoja huku katika michezo 6 akipoteza 1 na kufudhu robo fainal ya FA watacheza dhidi ya Southampton walio katika kinyang'anyiro cha kucheza Uefa mwakani.
   Watamkosa Morrison huku Anichebe akirejea wakati Soton wataendelea mkosa Toby,J.Rodriguez
   Tutaraji mchezo mgumu sana kutokana na aina ya uchezaji kwa pande zote,Soton wanacheza kwa spidi sana huku wenyeji wao maranyingi wanalinda goli na kufanya mashambulizi ya kustukiza pia katika michezo 3 iliyopita W.brom hawajafunga goli mbele ya Soton.


NB::West Brom imefunga magoli mengi 8 kutokana na kona zaidi ya timu zote katika ligi ukiwaondoa Chelsea walio sawa .
  -Katika michezo 7 ni mchezo mmoja tu ndo golikipa Foster karuhusu goli chini ya T.Pulis.
_______________________________________________________

GRANADA vs BARCELONA 18:00                 
  Los Carmenes uwanja wa nyumbani wa Granada walio chini ya Abel Resino watakwaana na wababe wa Man City,Fc Barcelona.
   Katika mchezo uliofanyika Camp Nou tulishuhudia Barcelona wakishinda 6-0 huku Neymar akifunga magoli matatu vijana hawa wa Resino watamkosa mshambuliaji wao tegemezi Youssuf-El Arabi huku Colunga akiwa majeruhi.

   Barcelona wao watamkosa Pique baada ya kufungiwa huku Mathieu akitarajiwa chukua nafasi ya mkongwe huyo.
   Baada ya kufungwa na Malaga goli la mapema kabisa na kusimamisha ushindi wa michezo 11 mfululizo katika mashindano mbalimbali  kinaweza kuwapa kujiamini kwa Granada kufanya vyema katika mchezo huu ambao Barca wakipoteza itawapa fursa Real kutanua wigo wa pointi dhidi yao.


    MSN kombinenga baada ya kufanya vyema Uefa watataraji endeleza moto walio uwasha tangu mwaka uanze huku Messi akitafuta goli 3 kumfikia Cristian Ronaldo..
  Ngoja tusubiri kama Granada walio nafasi ya 19 watashinda ilikujinasua na kushuka daraja kingine tutaraji kujilinda zaidi kwa Granada na mashambulizi ya kustukiza dhidi ya Barca walio nafasi ya 2.


NB:: Katika michezo 7 iliyopita Granada wameshinda mchezo 1 dhidi ya Barca.

_______________________________________________________


Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa uchambuzi makini katika masuala mbalimbali hususan michezo.

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

 Imeandaliwa na................
                                                Mr CHOI
                                             Choikangta.ckt@gmail.com
                                               WhatsApp -0765 691418

0 comments:

Post a Comment