Ni baada ya Polisi Kuuwa Raia.Inasemekana polisi walivamia eneo la kilabuni na kuanza kupiga kila raia
na kusababisa kifo cha huyo mama muuza Pombe za kienyeji. Kosa ni
kufungua kilabu cha Pombe kabla ya muda ulioruhusiwa kisheria.
Wananchi wamechoma matairi barabara Kuu hakuna gari inayopita, Polisi
bado hawajafika waliopo wamekimbia baada ya kuzidiwa na wananchi.
Sasa hivi wananchi wanaandamana kwenda kuchoma moto kituo cha polisi.Gari tatu zilizosheheni FFU zimewasili mabomu yanapigwa mfululizo, sasa
hivi wanasafisha barabara kwa kuzima moto na kutoa matairi njiani.
Wananchi Walioenda kituoni wamechoma moto matairi na magari mabovu yaliyopakiwa kituoni.
UPDATES
WANANCHI wenye hasira mjini Ilula,
mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha
kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari
yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake
kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia
polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.
Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto
magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari
kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.
Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kituo cha polisi cha Ilula mkoani Iringa kimechomwa na wananchi wenye hasira kufuatia polisi kumuwa mwanamke mmoja mfanyabiashara ya mama
ntilie wakati wa msako maalum ulioendeshwa na jeshi la polisi dhidi ya
wafanyabiashara hao.Inasemekana wakati wa purukushani za kukimbia
ndipo polisi mmoja alimchota mtama huyo mama wakati anakimbia na kusababisha mama wa watu kuanguka na kufariki hapo hapo.
Source: Radio Couds
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
0 comments:
Post a Comment