Wednesday, 25 February 2015
UCHAMBUZI MECHI ZA LEO JUMATANO LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA NA Mr.CHOI {KWA TAARIFA YAKO}
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
ARSENAL vs MONACO 22:45
Baada ya mechi za jana hii leo kipute cha Uefa kinaendelea vijana wa mzee Wenger watakapo chuana na Monaco iliyo chini ya Leonardo Jardims huku Leverkusen wakiwakabili Athletico Madrid.
Tukianzia katika dimba la Emirates Arsenal walio katika fomu hivi sasa licha ya kuwa na majeruhi kadhaa kama Arteta,Ramsey,Debuchy na Diaby watataka kuendeleza rekodi yao nzuri mbele ya timu za Ufaransa kwani mara ya mwisho kufungwa nyumbani na timu za Ligue ¹ ilikuwa msimu wa 2002/3 katika hatua ya makundi baada ya kufungwa 2-1 na Auxerre pale Highburry.
Kama ilivyo kawaida falsafa ya Wenger ni kushambulia zaidi hivyo bila shaka watafanikisha malengo yao katika mchezo wa leo kwa silaha za Sanchez,Cazorla aliye katika kiwango bora.
Kumbuka Monaco ndiyo timu ya mwisho nchini Ufaransa kufanya vyema katika michuano hii baada ya kutinga fainali mwaka 2004 na kupoteza mbele ya Porto ya Mourinho kwa kufungwa 3-0.
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Tegemezi lao ni Berbatov aliye kipiga Spurs na Man United pia Yannick Ferreira Carrasco,Moutinho na Silva tutarajie mashambulizi ya kushtukiza na katika michezo saba ya ugenini katika Uefa hawajashinda zaidi ya kutoa sare mbili na kupoteza michezo mitano.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
BAYERN LEVERKUSEN vs ATLETICO MADRID 22:45
Pale Bay-Arena Leverkusen walio chini ya Roger Schimidt's
watacheza dhidi ya A.Madrid wanafainali wa msimu uliopita.
Mara ya mwisho kufuzu hatua ya robo fainal kwa Leverkusen ni msimu wa 2002 walipotinga fainal na kupoteza mbele ya Real Madrid katika fainali iliyofanyika Hampden park jijini Glasgow-Scotland.
Watamkosa Toprak,Kruse,Jedvaj na Bender huku wapinzani wao wakiwa na mashaka kama Tiago atacheza.
Mara ya mwisho timu hizi kukutana ni msimu wa 2010/11 katika michuano ya Uefa ndogo na matokeo yalikuwa 1-1 kwa mechi zote tegemezi la Leverkusen ni Drmic huku wapinzani wao wakijitapa kwa safu nzuri ya Griezman na MandzukiƧ.
Tutaraji mchezo wa kasi kulingana na uchezaji wa timu zote.
------------------------------------------------------------------------
Usikose kuangalia mechi zote za leo kupitia SIMU,TABLET au COMPUTER yako kwa msaada wa BantuTz LIVESTREAMING.Tutakuletea links za mechi hiyo hivi punde hapa hapa www.bantutz.com
------------------------------------------------------------------------------------------------
Imeandaliwa na................
CHOIKANGA
Choikangta.ckt@gmail.com
WhatsApp -0765 691418
------------------------------------------------------------------------------------------------
0 comments:
Post a Comment