Facebook

Wednesday, 20 August 2014

Barcelona yafungiwa kusajili hadi mwaka 2016,FIFA yaipiga chini rufaa yao.


Barcelona hawataweza kusaini Mchezaji mpya
hadi Januari 2016 baada ya Dirisha la Uhamisho
la sasa kufungwa hapo Agosti 31 baada ya FIFA
kuitupa Rufaa yao ya kuzuiwa kufanya Uhamisho
wowote.

Barcelona iliadhibiwa Mwezi Aprili na FIFA
kutosaini Mchezaji mpya yeyote baada ya
kupatikana na hatia ya kukiuka taratibu za
kusaini Wachezaji wa Kimataifa walio chini ya
Miaka 18.

Hata hivyo adhabu hiyo ilisimamishwa ili
kuisikiliza Rufaa yao na hivyo Barcelona
kufanikiwa kusaini Wachezaji 8 wapya, akiwemo
Luis Suarez, kwenye Dirisha la Uhamisho la sasa.

Kurudishwa kwa Adhabu hii kunamaanisha kuwa
Barca haitaweza kusaini wachezaji wapya Mwezi Januari
Dirisha la Uhamisho likifunguliwa na lile
linalofuatia la Miezi ya Julai na Agosti 2015.

Hata hivyo, Barcelona imesema itakata Rufaa kwa
Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, CAS [Court
of Arbitration for Sport] kupinga Adhabu hii.

Hivi sasa Barcelona wako huru kumsaini
Mchezaji yeyote mpya hadi ifikapo

WACHEZAJI WAPYA WALIOCHUKULIWA KIPINDI
HIKI:
-Luis Suarez (Straika) - £75m kutoka Liverpool
-Marc-André ter Stegen (Kipa) - kutoka Borussia
Monchengladbach
-Thomas Vermaelen (Beki) - £15m kutoka Arsenal
-Jeremy Mathieu (Beki) - £15.8m kutoka Valencia
-Claudio Bravo (Beki) - £7.2m kutoka Real
Sociedad
-Jordi Masip (Beki) – Kapandishwa toka
Barcelona B
-Ivan Rakitic (Kiungo) - kutoka Sevilla
-Rafinha (Kiungo) – Alikuwa kwa Mkopo

Pamoja na Kifungo hiki cha kutofanya Uhamisho
wa Mchezaji yeyote pia Barcelona imepigwa Faini
Pauni 305,000 na kutakiwa na FIFA kurekebisha
kasoro za Usajili wao wa Wachezaji Chipukizi.
Pia, Shirikisho la Soka la Spain, RFEF, nalo
limepigwa Faini Pauni 340,000 kwa kutosimamia
vizuri Usajili huo wa Barcelona na pia kutakiwa
kurekebisha kasoro za kusimamia Usajili wa
Wachezaji Chipukizi.

Kiini cha adhabu hii ni uchunguzi wa FIFA
uliohusu Uhamisho wa Wachezaji 10 wa
Kimataifa walio chini ya Miaka 18 waliohamia
Barcelona na ambao walikiuka taratibu za FIFA.

Kwa mujibu wa Sheria za FIFA, Uhamisho wa
Wachezaji wa Kimataifa unaruhusiwa tu ikiwa
Mchezaji amevuka Miaka 18 na akiwa chini ya
hapo ni lazima atimize moja ya Masharti Matatu.
Kwanza, Mchezaji chini ya Miaka 18 anaruhusiwa
kuhamia Klabu ya Nchi nyingine ikiwa tu Wazazi
wake wamehamia huko kwa sababu zisizohusiana
na Soka [Yaani Wazazi hao wasihamie Nchi
nyingine kwa sababu tu Mtoto wao anahamia
Klabu mpya].

Pili, Mchezaji chini ya Miaka 18 anaruhusiwa
kuhamia Klabu ya Nchi nyingine ikiwa Nchi hizo
zipo mbili kwenye Jumuia ya Nchi za Ulaya.

Tatu, Mchezaji chini ya Miaka 18 anaruhusiwa
kuhamia Klabu ya Nchi nyingine ikiwa Klabu hiyo
ipo ndani ya Kilomita na anapoishi.

Licha ya FIFA kutangaza kuwa Barcelona ilikiuka
Sheria hizo lakini ilikataa kuwataja Wachezaji hao
Chipukizi wanaohusika kwa kudai hiyo ni siri.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata habari mbalimbali kwa muda na wakati muafaka.

0 comments:

Post a Comment