Wednesday, 20 August 2014
Manchester United yamnasa ramnasa rasmi "beki kisiki"Marcos Rojo.
Manchester United imetangaza rasmi kumsaini Beki wa Sporting Lisbon,Marcos Rojo kwa ada ya Euro Milioni 20 na kumpa
Mkataba wa Miaka Mitano.Kwenye dili hiyo,Luis Nani amekwenda Sporting Lisbon kwa Mkopo wa Msimu mmoja.
HISTORIA YA ROJO KATIKA SOKA
Rojo, mwenye Miaka 24, alihamia Sporting Lisbon Mwaka 2012 akitokea Spartak Moscow.Beki huyo alicheza Mechi zote za Argentina huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia, na kufunga goli 1 dhidi ya Nigeria, na Argentina kufika Fainali iliyofungwa Bao 1-0 na Germany.Umahiri wake ulimfanya awemo kwenye Timu ya FIFA ya Fainali za Kombe la Dunia za Brazil 2014.Kabla ya kuhamia Spartak Moscow na kisha Sporting
Lisbon, Rojo aliichezea Estudiantes ya Argentina na kutwaa Copa Libertadores Mwaka 2009.Mara baada ya kukamilisha Uhamisho huu, Rojo alisema:
“Ni heshima kubwa sasa kutamka naichezea Manchester United. Ligi Kuu England ni Ligi kubwa Duniani na kupata nafasi kuichezea Klabu kubwa kabisa Duniani ni ndoto kwangu.Mimi bado Kijana na nina ari kuendelea kujifunza na kucheza chini ya Kocha mzoefu Louis van Gaal!”
Nae Meneja wa Manchester United,Louis van Gaal alikuwa na haya ya kusema:“Marcos ni Beki mwenye kipaji. Amecheza Soka la kiwango cha juu kabisa na anaweza kucheza kama beki wa kati au beki wa Kushoto. Ana uwezo,nguvu na nia ya kujifunza na hii inamaanisha mwisho wake ni mzuri. Alicheza vizuri kwenye Kombe la Dunia na amecheza Ulaya kwa Miaka kadhaa sasa. Ni nyongeza nzuri kwa Timu!”
Katika mtandao wa kilabu ya Manchester United (manutd.com) wameandika hivi;
" Manchester United is delighted to announce the signing of
defender Marcos Rojo on a five-year contract from Sporting
Lisbon for a fee of €20 million, with Nani joining the Portuguese
club on a season-long loan."
Endelea kutembelea www.bantutz.com uendelee kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na usajili.
0 comments:
Post a Comment