Thursday, 21 August 2014
Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu{HESLB} yahaidi kulipa fedha kwa Wanafunzi wa Vyuo vikuu,Walioomba mikopo nao kushughulikiwa.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB),imesema mwishoni mwa wiki hii, itakuwa imelipa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ambao hawajapata fedha hizo kwa mwaka 2013/14.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, aliyasema hayo Dar es Salaam
jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/15.
Alisema bodi hiyo ilikwama kuwalipa baadhi ya wanafunzi walioanza mafunzo kwa vitendo Julai mwaka huu kutokana na
uhaba wa fedha.
Aliongeza kuwa, hadi sasa vyuo vitano ndivyo ambavyo wanafunzi wake hawajapatiwa fedha hizo, lakini hadi mwishoni mwa wiki hii, fedha hizo zitakuwa zimeingizwa kwenye akaunti zao.
Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo cha Tumaini Makumira Arusha (TUMA), Chuo cha Mtakatifu Stefano Moshi (SMMUCO),Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mtakatifu Agustine Mwanza na Chuo cha Theophil Kisanji (TEKU), ambapo jumla
yao wapo wanafunzi 9,946.
Katika hatua nyingine, Mwaisobwa alisema hadi wanafunga maombi ya mikopo Julai 31 mwaka huu, wamepokea maombi yamikopo 58,037 kati ya hiyo, wavulana 37,689 na wanawake 19,592,” alisema.
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata kila taarifa itakayokuwa inahusiana na mikopo kwa wanafunzi wa Vyuo vikuu nchini.
Guud
ReplyDelete