Facebook

Thursday, 21 August 2014

Unyama !! Kijana amkata kichwa Mdogo wake ili apate utajiri huko Morogoro

 
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni!
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro
linamng’ang’ania mfanyabiashara maarufu
wa Wilaya ya Mvomero, Johnson Damian
Mkude (39) akituhumiwa kumkata kichwa
mdogo wake wa kuzaliwa, Mathias kisha
kuondoka nacho kwenda kwa mganga kwa
kile kilichodaiwa ni kufanyiwa dawa ili awe
bilionea,
Tukio hilo ambalo kwa sasa ndiyo gumzo
mkoani hapa lilijiri usiku wa Agosti 3,
mwaka huu katika mashamba ya Kata ya
Mlali ambapo ndugu wa marehemu
waliokuwa wakimsaka ndugu yao
walifanikiwa kuona kiwiliwili Agosti 6,
mwaka huu.
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya
Nyandila (Chadema), Peter Joseph Zengwe,
Agosti 15, mwaka huu baada ya mauaji
hayo kutokea, vijana wawili, Amos na
Mohamed Chali walikamatwa na polisi
wakidaiwa kuhusika na mauaji hayo.
“Siku chache baada ya mauaji hayo, Amos
na Mohamed Chali walifuja pesa kwa
kunywa pombe kupita kiasi ambapo mmoja
aliropoka kilabuni kwamba walilipwa fedha
nyingi kwa kumuua Mathias.
“Baada ya majigambo hayo, watu wakatoa
taarifa polisi na wahusika wakakamatwa na
ndiyo waliomtaja Johnson,”

0 comments:

Post a Comment