Jeshi la Uganda UPDF limesema linapanga kuanza kuandaa michuano ya kutafuta mrembo wa taifa - Miss Uganda beauty contest.
Mshauri wa rais wa masuala ya kijeshi Jenerali Caleb Akwandwanaho - maarufu kama Jenerali Salim Saleh (mdogo wake Rais Yoweri Museveni) amesema hatua hiyo ina lengo la "kuvutia vijana katika sekta ya kilimo",
Akiongeza kuwa itasaidia katika kutatua "matatizo ya njaa na umasikini miongoni mwa vijana nchini humo," limeripoti gazeti la Daily Monitor.
Akandwanaho amesema jeshi pia lipo katika mchakato wa kusimamia kilimo nchini humo, ili kuondokana na ukulima wa kujipatia chakula tu hadi kuwa ukulima wa kibiashara. Kufanikisha hilo watu zaidi wanatakiwa kuanza kupenda kilimo,amesema.
Lakini hatua ya UPDF kuingia katika kilimo cha biashara na mashindano ya urembo imeshangaza baadhi ya watu. Waziri mmoja ameonya maafisa wapya wa jeshi waliopewa mafunzo ya kilimo kutojihusisha na ufisadi.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wanadhani jeshi, kilimo na mashindano ya ulimbwende hayaleti maana yoyote. "Itafanyaje kazi? Je warembo watafanya maonesho yao juu ya matrekta?" ameuliza mmoja wa watu katika mitandao ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment