Facebook

Wednesday, 20 August 2014

MAAJABU YA DUNIA:BINADAMU AGEUKA MTI


Ni miujiza ya Mungu. Mitihani ipo
kila kona kwa aina mbalimbali lakini
hatutakiwi kukufuru. Tunapaswa
kukubali matokeo na kuomba nusura
kwa Muumba, kwani kazi yake haina
makosa.
Binadamu ageuka mti! Unaweza
kudhani ni simulizi ya miujiza lakini
huo ndiyo ukweli. Ndugu yetu
anayeitwa Dede Koswara, 41, raia wa
Indonesia hivi sasa hatamaniki na
wengi wanamwita ‘nusu mtu, nusu
mti’.
Dede hajarogwa, isipokuwa amepata
maradhi hayo baada ya
kushambuliwa na virusi hatari
wanaoitwa Human Papilloma (HPV),
hivyo kubadili kabisa muonekano
wake.


HALI HALISI YA DEDE
Alianza kushambuliwa na virusi hivyo
akiwa na umri wa miaka 17, kwa
maana hiyo ni tatizo ambalo ameishi
nalo kwa miaka 24 sasa.
Ugonjwa ulianza kumshambulia
kwenye mikono na miguu kabla ya
kuhamia maeneo mengine ya mwili
wake mpaka kichwani.Tatizo ni
kubwa kiasi kwamba vioteo vya
upande wa mikono na miguu,
vinashabihiana na miti mikavu, ubao
mkavu ambao haujaondolewa
magome yake.
Alishafanyiwa upasuaji mara tisa
kuondoa tatizo hilo lakini mafanikio
yakawa kupunguza kwa asilimia 95
kabla ya kuanza kuota tena.
Viotea ambavyo vinamfanya Dede
aonekane kama mti, kitaalamu
vinaitwa mapembe (cutaneous
horns).
Hupatwa na maumivu makali
kutokana na hali hiyo, hivyo
kumfanya ashindwe kutembea au
kufanya lolote lile.
Januari, 2008, akiwa na umri wa
miaka 37, alifanyiwa upasuaji wa
kwanza. Alipata nafuu na kueleza:
“Namshukuru Mungu, angalau
naweza hata kutembea.”
Alipopatwa na maradhi hayo, alikuwa
anajishughulisha na kazi za uvuvi
lakini kwa sasa ameshindwa kumudu.




 
NGUMU KUPONA
Dk. Rachmad Dinata
wa Hospitali ya Hasan Sadikin,
Indonesia, amesema: “Hawezi kupona
kwa asilimia 100 lakini maisha yake
yanakuwa bora. Tumemtibu na
kupunguza ukali wa ugonjwa, alikuwa
anategemea watu kumfanyia kila kitu
lakini sasa anaweza kula yeye
mwenyewe, kuandika na kutumia
simu ya mkononi.”


Dk. Anthony Gaspari, raia wa
Marekani anayetokea Chuo Kikuu cha
Maryland, amejitolea kufanya utafiti
kubaini tiba kamili ya ugonjwa wa
Dede. Taarifa yake ya awali, imeeleza
kuwa virusi hao ambao ni adimu
duniani, wamemfanya Muindonesia
huyo aishiwe kabisa na kinga za
mwili.
Dede ameweka tumaini lake kwa
daktari huyo wa Marekani na
ameeleza: “Naamini nitapona ila sijui
lini. Kuna siku nitakutana na
mwanamke na nitafunga naye ndoa.
Natamani niwe baba wa familia na
baadaye niwe na watoto. Napenda
sana nibaki hai mpaka
nitakapowaona wajukuu.”

0 comments:

Post a Comment