Facebook

Wednesday, 20 August 2014

Picha: Mama mzazi wa Sylvester Stallone 'Rambo' mwenye miaka92 akifanya mazoezi yakunyanyua vyuma


Kama ulimuona Sylvester Stallone kwenye
Expandables, bila shaka uliona umri wake
ulivyo mkubwa huku akiendelea kutisha kama
bado ni kijana mdogo. Sasa utamshangaa zaidi
mama yake mzazi, Jackie mwenye miaka 92
anaeamini umri sio kikwazo.





Bibi huyo ameendelea kufanya mazoezi ya
viungo licha ya kuwa na umri mkubwa na hata
anapokuwa gym hubeba hadi vyuma vyenye
uzito huku akisaidiwa kwa ukaribu na watu.


 
 Bibi Jackie bado anavaa Mini-Skirt, na kupaka
make up kama wanavyofanya wasichana
warembo wenye umri mdogo.



 
“Hollywood wanahofia umri, lakini nadhani
wazee ndio wanakuja. Nadhani umri wa
mwanamke wa kati unarudi. Wote tungependa
kufika kule, kufika kule kama mimi. Sio kwenye
kiti cha kukusaidia kutembea, wala kuwa
kwenye kitu maalum cha kutunzwa.” Amesema
mama Rambo.


Bi Jackie akiwa gym. 

0 comments:

Post a Comment