Kwa taarifa zilizotufikia kutoka Tabata jijini Dar es Salaam,ni kwamba,kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ujambazi katika eneo la tabata na kuhatarisha amani ya eneo hali iliyopelekea watu wa eneo hilo hususan Tabata-Luwiti kuchoshwa na vitendo hivyo.
Baada ya majambazi kuvamia maduka,sheli za mafuta na nyumba za wananchi wenye kipato kikubwa kisha kupora fedha na mali mbalimbali.
Asubuhi ya leo baada ya majambazi hao kutegewa mtego na wananchi wa Tabata-Liwiti na kisha,wakanasa,Ndipo wananchi wa eneo hilo wakiwa na hasira kali waliwazingira majambazi hao na kuanza kuwarushia mawe,kuwapiga na magongo makubwa hali iliyopelekea majambazi hao kuvuja damu na kupoteza fahamu.
Wananchi wa Tabata-Liwiti hawakuishia hapo waliwazungushia matairi ya magari kisha kuwamwagia mafuta aina ya Petroli na kuwachoma moto hadi kufa Papo hapo.
Alisikika mwananchi mmoja akisema "Wamezoea sana hawa,wanashindwa kufanya kazi za halali kujitafutia kipato wanakuja kutuvamia na kuanza kutupora mali zetu,lazma tuwaue tukomeshe tabia hii Tabata"
Endelea kutembelea www.bantutz.com upate habari kutoka kila kona kwa muda na wakati muafaka.
0 comments:
Post a Comment