Facebook

Wednesday, 6 August 2014

Yanga wafunguka baada ya kuondolewa kwenye Michuano ya Kombe la Kagame

Uongozi wa klabu ya Young Africans leo
umefanya mkutano na waandishi wa habari
juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa
michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza
sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno
Njovu amesema walipata barua ya mwaliko
wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014
na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa
kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao
kuiwasilisha kwa CECAFA.
"Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano
hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya
wachezaji na viongozi ambao watasafiri
kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano
hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na
sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza"
alisema Beno.
Lakini katika hali ya kushangaza jana
tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA
imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa
kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya
Azam kuchukua nafasi yetu "aliongeza Beno."
Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji
wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni
lazima wawe na leseni za kucheza mpira
kutoka kwa chama husika, jambo ambalo
ambalo orodha tuliyowapelekea wachezaji
wote wataichezea Yanga msimu huu wa
2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya
kikosi ambacho kingekwenda kushiriki
michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza
ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua
dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua
kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua
na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka
timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji
watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya
kocha Leonado Neiva ambaye amekua na
wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa
klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine
kwa kusema kikosi kilichopelekwa
hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu
Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya
kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo
Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho
kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu
uliopita Hans ilitoa maelekezo ya kupunguza
wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili
kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya
kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika
idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita.
b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na
majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa
Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19,
2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani
miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata
muda wa kupumzika.
c) Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia
kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake
watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda
na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda
wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye
timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha
kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.
d) Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya
kufanyia kazi nchini, uhamisho wa Kimataifa
(ITC) ili waweza kushiriki michuano ya
Kagame, na moja ya kanuni za CECAFA
mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni
lazima awe na leseni ya kucheza mpira kwa
ligi ya ndani.
e) Katika wachezaji 20 waliochaguliwa
kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6
wamepandishwa moja moja katika kikosi cha
wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi ya
wachezaji wa U20 kuwa watano tu.
f) Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars
kwa takribani miezi mitatu bila ya kupumzika,
daktari alipendekeza wapate japo siku kumi
na nne (14) za kupumzika ili miili yao iweze
kupoa na kuanza upya tena maandalizi ya
msimu mpya.
g) Yangga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi
ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi
cha kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na
wachezaji mda wote na kujua ubora wa
wachezaji wake.

0 comments:

Post a Comment