Facebook

Sunday, 2 November 2014

BRENDAN RODGERS ALIA NA LIVERPOOL, ATAKA STEVEN GERRARD APEWE MKATABA MPYA HARAKA

KOCHA wa Liverpool, Brendan
Rodgers anataka nahodha wake Steven
Gerrard aendelee kubaki klabuni na
anataka apewe mkataba mpya.

Gerrard amezua sintofahamu kupitia
mahojiano yake na Sportsmail siku ya
Ijumaa pale aliposema bado hajapewa
mkataba mpya Liverpool na anaweza
akachezea klabu nyingine msimu
ujao .

Mkataba wa sasa wa kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 34
unamalizika mwezi Juni mwaka ujao
na hii ni mara ya kwanza kwa
Gerrard kucheleweshewa mkataba
mpya katika klabu yake hiyo ya tangu
utotoni.

Katika mahojiano yake hayo, Gerrard
alisema: “Sitastaafu mwishoni mwa
msimu huu, nitaendelea kucheza
msimu ujao. Ni jambo la kusubiri na
kuona kama ni Liverpool au sehemu
nyingine yoyote. Hayo ni maamuzi ya
Liverpool.”

Hata hivyo Rodgers hakufanya siri
kuonyesha imani yake kwamba bado
Gerrard anatakiwa kuendelea kuwa
injini ya timu msimu ujao.

Kama Liverpool wataendelea kuwa
kimya kwa miezi miwili ijayo, Gerrard
ataruhusiwa kuanza kuzungumza na
timu zingine itakapofika mwezi
Januari, hii ikiwa ni kwa mujibu wa
sheria ya Bosman.

0 comments:

Post a Comment