Facebook

Friday, 14 November 2014

Equitorial Guinea kuandaa kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Taifa la Equitorial Guinea ndilo
litakaloandaa michuano ya dimba la
mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Kulingana na shirikisho la soka barani Afrika,
taifa hilo limetajwa baada ya Morrocco kukataa
kuandaa michezo hiyo kutokana na hofu ya
kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Morrocco ilikuwa imeiomba CAF kuahirisha
dimba hilo la January 17 hadi Feruary 8.
CAF vilevile imeipiga marufuku Morrocco
kushiriki katika dimba hilo ambalo sasa
litaandaliwa na taifa lililoandaa kombe hilo na
Gabon mwaka 2012.

Equitorial Guinea sasa itachukua jukumu lote la
kuandaa michuano hiyo yenye mataifa 16.
CAF imetangaza kuwa mechi hizo zitachezwa
katika miji minne ikiwemo Malabo,Mongomo
na Ebebiyin.Droo ya mechi hizo itafanyika
mjini Malabo tarahe 3 mwezi Disemba.
Haijabainika iwapo mwenyeji huyo mpya
atashiriki katika dimba hilo kwa kuwa timu
hiyo ilipigwa marufuku mwezi Julai kwa
kuchezesha mchezaji asiyetakikana katika
mechi ya kufuzu kwa dimba hilo dhidi ya
Mauritania mnamo mwezi May 17.

0 comments:

Post a Comment