Jeshi la Nigeria linasema kuwa
limelikomboa eneo la Chibok siku mbili
baada ya wapiganaji Waislamu, Boko
Haram, kushambulia mji huo.
Wasichana wa shule zaidi ya 200 walitekwa
kutoka Chibok mwezi wa Aprili.
Msemaji wa jeshi, General Olajide Laleye,
alieleza kuwa mji umekombolewa lakini alikiri
kuwa operesheni bado haikukamilika na
inaendelea.
Haikuelezwa hasara iliyopatikana.
Wapiganaji waliposhambulia Chibok siku ya
Alkhamisi, wakaazi waliwashutumu wanajeshi
kuwa walikimbia bila ya kupigana.
Chanzo:BBC News.
0 comments:
Post a Comment