Facebook

Tuesday, 18 November 2014

Mambo muhimu unayotakiwa kuyajua kuhusiana na kifo cha Nabii Elia aliyekuwa akijiita Mungu.


Baada ya kifo cha aliyekua kiongozi na muasisi wa
Kanisa la Pool of Siloam Nabii Eliya mungu wa
Majeshi a.k.a Adamu wa pili, gazeti la JIBU YA
MAISHA linalomilikiwa na kanisa la TAG limeandika
mambo machache ya kushangaza kuhusu kiongozi
huyo na kanisa lake hilo maarufu hapa nchini.

Nasi BantuTz.com tunanukuu kwa maslahi ya umma:

1. Idadaiwa sababu ya kifo chake ni kuchomwa na
msumari mkononi na akakataa kwenda hospitali
kwa sababu kanisa hilo haliamini ktk tiba za
hospitali.


2. Nabii Eliya alijiita Mungu wa Majeshi (kinyume
na maagizo ya MUNGU wa kweli ambaye hagawani
utukufu na wanadamu). Lakini nabii Eliya aliwahi
kusema hatakufa na hata alipokufa waumini wake
wanaamini hajafa bali amepaa mbinguni. (wengine
wameanza kushuhudia kuwa walimuona akipaa).


3. Nabii Eliya alikua anasema anaishi mbingu ya
saba na hapa duniani kilichopo ni taswira yake tu,ila yeye yupo Mbingu ya 7 na huwa anawahudumia
wafuasi wake akitokea huko mbingu ya 7.


4. Alikataa matumizi ya neno BIBLIA kanisani
kwake. Alitoa kava za Biblia na kuweka kava zake
zenye maandishi "Kitabu cha haki"


5. Alipinga kuwa siku za mwezi si 30 bali 28 na
akatengeneza Kalenda yake yenye siku 28
inayofuatwa na waumini wake wote.


6. Mwaka 2008 alipanga upya majira ya mwaka na
kuonesha kuwa mwanzo wa mwaka si January bali
March (Wao huita Aviv) na mwisho wa Mwaka si
December bali February (wao huita Adari).


7. Wanaamini Sikukuu ya Chrismass (kuzaliwa kwa
Kristo) sio tar.25 December bali tar.28 February.


8. Unapokua muumini wa kanisa hili hulazimika
kubadili majina yako yote maana wanaamini yana
laana hivyo hukupa majina mengine.


9. Waumini wa kanisa hili wanapomsalimia mtu
asiye muumini wao kwa kushikana mikono
hushauriwa kunawa mikono haraka sana baada ya
salamu, ili kuondoa mapepo yanayoweza kuwapata
kwa kushikana mikono.


10. Waumini wa kanisa hili wanaamini SHETANI
HAYUPO.. Shetani alishakufa. Na aliyemuua
Shetani ni Nabii Eliya.Wanaamini kuwa tar.4
Novemver 2008 Nabii Eliya alimkamata shetani
akampiga kabali na kumuua.Hivyo Shetani
hayupo hai tena.


Huyo ndo Adamu wa pili Nabii Eliya, Mungu wa
Majeshi ambaye majina yake halisi ni
NDUNAMINAMFOO MUNUO, Mchagga wa Moshi
Machame.Nafasi yake ya uongozi wa kanisa
imechukuliwa na mtu mmoja ajiitaye "Kuhani Eliya
Miaka Elfu moja.!"


R.I.P NDUNAMINAMFOO MUNUO.!!

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kujua kinachojiri katika sehemu mbalimbali.Hapa BantuTz.com utapata habari na stori zote.

0 comments:

Post a Comment