Facebook

Saturday, 15 November 2014

Kiongozi asiyekuwa na Choo,kupigwa chini India.

 
Jimbo la Gujarati nchini India linataka iwe
sheria kwa mtu yeyote anayetaka kuwania
wadhfa wa uma kuwa na choo nyumbani
mwake,ili kuzuia watu kwenda haja katika
maeneo yalio wazi.
Mswada uliopitishwa na bunge la Gujarati siku
ya jumatatu pia unataka viongozi
waliochaguliwa kubaini katika kipindi cha miezi
sita iwapo wana vyoo nyumbani la sivyo
waondolewe katika nyadhfa zao.
''Kukabiliana na watu wanaokwenda haja katika
maeneo ya wazi ni muhimu kwa lengo la
kuimarisha mazingira safi mbali na uchafuzi wa
maji','ilisema serikali.
Gujarat ni jimbo la nyumbani la waziri mkuu
mpya Narendra Modi ambaye amesema kuwa
kila nyumba ni sharti imiliki choo katika
kipindi cha miaka minne ili kuzuia magonjwa
yanayosababishwa na watu kwenda haja katika
maeneo ya wazi.

Mamilioni ya raia nchini India hawana vyoo.
Hatahivyo raia hao wanadaiwa kuwa na tatizo
la utumizi wa vyoo.hii ni kwa sababu kila
sekunde mtu mmoja huenda haja katika eneo
la wazi,swala linalosababisha ugonjwa wa
utapia mlo miongoni mwa watoto, kushuka
kwa uchumi pamoja na ghasia dhidi ya
wanawake.
Ni tatizo ambalo waziri mkuu Narendra Modi
ameamua kuhakikisha kuwa kila nyumba ina
choo ifikiapo mwaka 2019.
Lakini kulingana na wataalam wa usafi ,jibu
halitapatikana iwapo kutajengwa vyoo zaidi vya
kuogea ,kwanza raia ni sharti waanze
kupendelea kwenda katika vyoo.

0 comments:

Post a Comment