Facebook

Saturday, 15 November 2014

Chombo kilichotumwa na Wanasayansi kwenye kimondo chaishiwa nguvu ya umeme.

Wki iliyipita BantuTz tuliripoti kuhusiana na chombo kilichotumwa na wabasayansi katika kimondo hii ni taarifa nyingine iliyotufikia hivi pinde kuhusiana na chombp hicho.

Chombo cha anga za juu Philae kilichotua
katika nyota mkia "Kimondo" kimetuma tena taarifa
nyengine muda mfupi kabla ya kupoteza
nguvu za umeme.

Kila kilichotarajiwa kutoka kwa chombo hicho
kilipokelewa kabla ya kuonyesha kwamba nguvu
za umeme za chombo hichoo zimekwisha.

Chombo hicho kimezibwa na mwamba na
hakiwezi kupata mwanga wa jua ili kuchaji
betri yake.

Wahandisi wanahofu kwamba huenda taarifa
iliopatikana ndiyo ya mwisho kwa mda huu.

Chombo hicho kilitua katika sakafu ya nyota
mkia 'kimondo' siku ya jumatano,ikiwa ni mara ya kwanza
kwa chombo kilichotumwa katika anga za juu
kutua katika nyota mkia 'kimondo'.

Fursa nyengine ya kuwasiliana na Philae ni
wakati chombo cha Rosetta kilichopeleka
Philae katika nyota hiyo kitaonekana tena.

Huku Philae ikiweza kupata mwanga wa jua
kwa takriban jisaa moja na dakika hamsini
pekee, haijulikani iwapo battery yake itaweza
kupata nguvu ya kuendelea kutoa taarifa.

0 comments:

Post a Comment