Facebook

Wednesday, 12 November 2014

MTOTO MWENYE SEHEMU NNE ZA SIRI NA MIGUU YA AJABU AZALIWA,WAZAZI WAMTELEKEZA WODINI-ARUSHA.

 
AGANO kwamba nyakati za mwisho,
matukio mengi ya ajabu yatadhihirika,
linazidi kupata nguvu kutokana na tukio
la kusikitisha lililotokea Arusha.
Wakazi wa jiji hilo, wanaliita A-Town na
ukifanikiwa kushiriki vijiwe mbalimbali,
utabaini jinsi mkoa huo ulivyozizima
kutokana na kuzaliwa motto mwenye
sehemu nne za siri.

Kila kona ya jiji hilo, anazungumzwa
mtoto huyo kwa hali ya mshangao.
Malaika huyo wa Mungu hajapewa jina
lakini mama yake anaitwa Naishooki
Logolie, 23, mkazi wa Kijiji cha Injok,
Wilaya ya Arumeru, Arusha.
Kutokana na habari ya mtoto huyo
kupata umaarufu mkubwa, huku wengi
wakitaka kumjua zaidi,ripota wa BantuTz mkoani Arusha  alimsaka
mtoto huyo na kubaini maajabu
mengine kwamba mbali na sehemu hizo
za siri pia ana miguu mgongoni.
Kwa ushuhuda wa ripota huyo, mtoto huyo ni
wa kiume lakini ana sehemu za siri nne,
tumboni, mgongoni, ubavuni na kwenye
eneo la kawaida.


KAULI YA MAMA MZAZI
Ripota wa BantuTz alifanikiwa kuzungumza na
Naishooki ambaye alisema: “Mwanangu
nilimzaa kwa njia ya upasuaji kwenye
Hospitali ya Olturumet, Halmashauri ya
Arusha.”

 
Naishooki alisema hajui ni mtihani gani
umempata kwani hakuwahi kuhisi tatizo
lolote tumboni. Baada ya hapo,
mwanamke huyo aliangua kilio na
hakuweza kuzungumza tena.
Mama mzazi wa mtotot huyo.
Mama mzazi wa Naishooki (bibi wa
mtoto huyo), Naishiye Logolie, alisema
kuwa ni tukio la ajabu mno kutokea.
“Mtoto wangu akiwa mjamzito,
hakuwahi kuonesha dalili za tatizo.
Tumeshangaa kuona maajabu haya,”
alisema Naishiye.


KAULI YA DAKTARI
Akizungumza na waandishi wa habari,
Mganga wa Halmashauri ya Arusha,
Dk.Thobias Mkina alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kusema kuwa
wanajaribu kufanya linalowezekana
kuokoa maisha ya mtoto huyo.
“Matukio ya kuzaliwa watoto wakiwa na
matatizo yanatokea lakini hili kidogo
linaonekana kuwa la kipekee sana
kutokana na maumbile ya mtoto,”
alisema Dr.Mkina.
Alisema kuwa sababu za kitaalamu
zinazoweza kusababaisha matukio ya
aina hiyo ni matumizi ya dawa zenye
kemikali wakati mama akiwa mjamzito.
Dokta huyo aliongeza, wakati mwingine
kuna matukio ya kurithi kutoka kwa
kizazi cha mhusika.
Hata hivyo alisema uchunguzi
unaendelea na wakimaliza kwa upande
wao watampatia rufaa kwenda katika
hospitali kubwa zaidi.

MTOTO ATELEKEZWA
Taarifa za baadaye zinasema kuwa
mtoto huyo aliepelekwa Hospitali ya
KCMC, Moshi, Kilimanjaro kwa lengo la
kufanyiwa upasuaji lakini wazazi hao
baada ya kuambiwa gharama,
walimtelekeza wodini.

BantuTz tumejiridhisha kuwa mtoto huyo
ametekezwa wodini kwenye hospitali
hiyo, huku wazazi wake wakisema kuwa
hawawezi kuishi na kiumbe huyo kwa
madai kwamba ni laana kutoka kwa
Mungu.


BantuTz.com inawashauri wazazi wa
mtoto huyo kurudi KCMC kumchukua
mtoto huyo. Kiumbe huyo ni malaika na
hana kosa lolote.

BantuTz.com  tunaendelea
kumfuatilia mtoto huyo hatua kwa hatua
na tutakuwa tunatoa ripoti ya
maendeleo kutoka kwa ripota wetu aliye Arusha.



Imeandaliwa na........ 
                                   Mfariji Katemi Peter.

0 comments:

Post a Comment