Facebook

Friday, 14 November 2014

Mwizi akamatwa akiwa ameficha nyama sehemu za siri-Dar es Salaam

Ukistajaabu ya Musa utayaona ya Firauni.

Hivi punde BantuTz tumepokea taarifa kutoka kwa ripota wetu aliye maeneo ya Magomeni kwamba kuna mwizi amekatawa katika 'Pub' moja maarufu sana maeneo hayo kwa uchomaji wa nyama ya Nguruwe 'Kitimoto'.Pub hiyo imeomba jina lake lisitajwe.

Cha kustaajabisha ni kwamba mwizi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa amekamatwa akiwa ameficha baadhi ya vipande vya nyama hiyo takribani kilo moja na nusu katika sehemu zake za siri.

Mwizi huyo baada ya kukamatwa amepewa masharti mawili,achague moja;Apigwa na wananchi au apigwe picha zitakazosambazwa mtandaoni na kisha kupelekwa polisi.

Mwizi huyo amechagua kupigwa picha akiwa ameziweka nyama hizo sehemu za siri na kisha kupelekwa polisi.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata taarifa na stori mbalimbali kutoka kwa maripota wetu waliosambaa kila sehemu.

Ameiba nyama ya kitimoto kwenye pub akaificha kwenye mapumbu. Raia wamemwambia achague miwili ale kipondo au akubali kupigwa picha za ushahidi na apelekwe polisi. Akachagua kupiga picha na kupelekwa polisi kama sehemu ya masharti ya msamaha. Mwenye pub ametusambazia wajumbe wote wa bodi picha za tukio kwenye whatsapp

0 comments:

Post a Comment