Kanda moja ya video iliowekwa mtandaoni
inaonyesha mauaji ya mtu wa kutoa
huduma za misaada raia wa Marekani Abdul
Rahman Kassig ambaye alikuwa
anajulikana kama Peter Kassig kabla ya
kutekwa nyara na wanamgambo wa Islamic
State nchini Syria mwaka uliopita
Video hiyo inamuonyesha mawanamume
mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa
Islamic State akiwa na kisu mkononi na
maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig
ameuawa.
Kanda hiyo pia ina picha za watu kadha
waliouawa ambao wanasemekana kuwa
wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa
nyara.
Marekani imesema kuwa inafanya juhudi za
kubaini chimbuko la kanda hiyo.
Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter
alitekwa nyara mwaka uliopita.
Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video
ya kifo cha mfanyikazi mwengine wa misaada
kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku
Kassig akitishiwa.
0 comments:
Post a Comment