Mchezaji Lukas Podolski wa Ujerumani alilichezea
taifa lake kwa dakika 90 dhidi ya Gibraltar
siku ya ijumaa lakini anashangazwa kuona
ni kwa nini hajaanzishwa kuichezea kilabu
yake ya Arsenal.
Lucas
Podolski anasema kuwa mkufunzi wa kilabu
hiyo Arsene Wenger anampuuza.
Mshambuliaji huyo amechezeshwa mechi nne
pekee katika ligi ya Uingereza msimu huu,huku
akianzishwa katika mechi ya kombe la Carling
ambapo Arsenal ilipoteza kwa Southampton
mnamo mwezi Septemba.
Lucas Podolski alicheza dakika 90 wakati
Ujerumani ilipoicharaza Gibraltar mabao 4-0
katika mechi za kuwania kufuzu katika dimba la
Ulaya,lakini mkufunzi Joachim Low anataka
mchezaji huyo kuanza kuchezeshwa mara kwa
mara katika kilabu yake.
Mchezaji huyo aliyetoka kilabu ya Koln nchini
Ujerumani alisema kwamba anapanga kufanya
mazungumzo na Arsenal kuhusu hatma yake
mwezi january na akasisitiza tena siku ya
ijumaa wakati taifa lake liliposhinda.
''Nimekuwa nikiichezea Arsenal kwa dakika
chache ,niko tayari kuionyesha Arsenal kile
naweza kuifanyia ,lakini fursa hiyo
haipatikani'',alisema Podolski.
CHANZO:BBC Sport.
0 comments:
Post a Comment