Facebook

Saturday, 8 November 2014

UCHAMBUZI:LIVERPOOL vs CHELSEA

TAREHE 8 NOVEMBA 2014
LIGI KUU YA UINGEREZA
LIVERPOOL  V  CHELSEA
ANFIELD
Saa 9:45 alasiri:

HABARI ZA KILA TIMU KWA UFUPI:

Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard anatarajiwa kuanza kwenye mechi ya Leo baada ya kuanzia benchi kwenye mechi iliopita dhidi ya Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Raheem Sterling, Jordan Henderson, Philippe Coutinho, Dejan Lovren na Mario Balotelli wote wanaweza kuanza lakini Daniel Sturridge bado yupo nje kwa kuwa ni majeruhi.

Mshambuliaji Diego Costa wa Chelsea anaweza kuanza mechi ya leo licha ya kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kilichotajwa juzi ili aweze kupona kutoka kwenye majeraha yake ya mara kwa mara ya nyama za paja.

Loic Remy, John Obi Mikel na Cesar Azpilcueta wote wanarudi kwenye mechi hii.

Remy na Mikel kila mmoja wametoka kwenye majeraha ya kinena na goti, wakati Azpilcueta atapatikana baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake ya mechi tatu.

TAKWIMU ZA MECHI:
USO KWA USO:

••• Chelsea wamepoteza mechi moja tu kati ya sita zilizopita kwenye Ligi Kuu na Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool.
Wameshinda tatu na kutoka sare mbili.

••• The Blues wanaweza kushinda mechi ya pili mfululizo Anfield (baada ya ile iliopita ya 2-0 mwezi April mwaka huu) ikiwa ndio mara ya pili kwenye historia yao.
Waliwahi kushinda hivyo mwaka 2003 na 2005 dhidi ya timu zilizokuwa kwenye wa juu kabisa.

••• Liverpool washawahi kupata ushindi mara nne mfululizo kwenye Ligi Kuu dhidi ya Chelsea.
Sasa leo hadithi ni kinyume chake. Leo Liverpool wanaingia uwanjani wakiwa hawajapata ushindi kwenye mechi nne mfululizo dhidi ya Chelsea. Wamefungwa 2 na kutoka sare 2.

Mpaka sasa ni wachezaji wanne tu ndio waliotengeneza nafasi nyingi za magoli msimu uliopita kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kuliko nafasi zilizotengenezwa na Cesc Fabregas wa Chelsea mpaka sasa kwenye msimu huu wa Ligi Kuu hiyo. Gerrard alitengeneza 13, Suarez 12, Lambert 10 na Rooney 10.
Fabregas ana 9 mpaka sasa na ana nafasi kubwa ya kuwapiku hao watu.

••• Ni timu tatu tu ndio zilizowahi kupata pointi nyingi zaidi ya Chelsea baada ya mechi 10 za mwanzo kwenye msimu mpya kwenye historia ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Timu hizo ni Manchester City ambapo kwenye msimu wa 2011/2012 waliweza kupata pointi 28 kwenye michezo 10 ya mwanzo wa Ligi Kuu, Chelsea hao hao nao waliweza kupata pointi 28 msimu wa 2005-2006 na Newcastle United nao walipata pointi 27 msimu wa 1995-1996.

LIVERPOOL:
••• Wana clean sheet mbili tu kwenye mechi 16 zilizopita za Ligi Kuu.

••• Wameshinda mechi 2 tu katika mechi zao 7 zilizopita za Ligi Kuu.

••• Kikosi cha Brendan Rodgers kina pointi chache kwenye hatua hii ukilinganisha na msimu uliopita.
Msimu uliopita mpaka hatua hii Liverpool walikuwa wana pointi sita zaidi, hivyo kwa sasa wana pungufu ya pointi sita kulinganisha na msimu uliopita.

••• Liverpool waliwahi kuwa na pointi chache kwenye hatua kama hii (yaani baada ya idadi za mechi 10) kwenye misimu minne ya Ligi Kuu ya Uingereza, na mara zote walimaliza msimu  wakiwa nje ya nne bora (Top Four).
Misimu hiyo ni; 1992/1993 nafasi ya 6, 1993/1994 nafasi ya 8, 2010/2011 nafasi ya 6 na 2012/2013 nafasi ya 7.

••• Kuna misimu mitatu, Liverpool waliwahi kuwa na pointi kama hizi hizi walizonazo sasa (pointi 14) kwenye mechi 10, lakini waliweza kusonga mbele na kumaliza kwenye top four.

••• Mario Balotelli amecheza dakika 689 bila kufunga goli kwenye Ligi Kuu ya Uingereza tokea alipofunga goli łake la mwisho kwenye Ligi Kuu hiyo.

CHELSEA:
••• Chelsea hawajafungwa kwenye mechi 13 zilizopita za Ligi Kuu. Wameshinda 10 na wametoka droo mechi tatu.

••• Vijana wa Jose Mourinho hawajaweza kupata clean sheet kwenye mechi sita za zilizopita za ugenini kwenye Ligi Kuu.
Mechi yao ya mwisho kupata clean sheet ugenini, ilikuwa dhidi ya Liverpool mwezi wa nne kwenye ushindi wao wa 2-0 pale Anfield

... Vijana hao wa Mourinho ndio timu kali kwenye mashambulizi huku wakifunga 23% ya nafasi walizojaribu.

••• Chelsea wamefunga magoli manne kwenye dakika 15 za kwanza z mchezo kwenye Ligi msimu huu kuliko timu yoyote kwenye nafasi za juu.

0 comments:

Post a Comment