Facebook

Saturday, 8 November 2014

Je ulijua kama Kondo la Nyuma au 'Placenta' huliwa?

Baadhi ya wanawake wanakunywa maji ya
Kondo la Nyuma saa chache baada ya
kujifungua

Hugeuka kuwa uchafu pindi mama
anapojifungua , sasa kwa nini baadhi ya
wanawake wanaamua kula Kondo la nyuma
au Placenta ikiwa mbichi ?
Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa
mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo
humsaidia mtoto kupata chakula na hewa
kutoka kwa mama akiwa tumboni.
Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la
Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa ,
lakini sio kila mtu ana mtazamo huu.
Baadhi ya wanawake wanaamini kuwa madini
yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi kwa
mtoto ili kumuwezesha mtoto kukuwa huwa
bado yanaweza kutumika na kwamba sio vizuri
kuitupa.
Wanasema kuwa mama bado anaweza kupata
madini muhimu wakati anapoendelea kupata
nafuu baada ya kujifungua na pia anapoanza
kuonyonyesha kwa kula Kondo la nyuma.
'Mama ale Kondo la Nyuma?'
Baadhi ya wanawake husaga kondo hilo na
kunywa maji yake saa chache tu baada ya
kujifungua, baadhi wanaihifadhi na kutengeza
tembe ambazo wanameza na wengine
wanaikata vipande vipande kwa kuweka chini
ya ndimi zao.
Wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa tembe hizo
zinaweza kuwapa nguvu na pia kusaidia maziwa
ya mama kuongezeka.
Kampuni moja nchini Uingereza inayotengeza
biadhaa mbali mbali kutoka kwa Kondo la
Nyuma, hulipisha watu kati ya pauni 150 au
dola elfu kumi na saba kwa kila tembe na chini
ya dola hamsini kwa maji ya kondo hilo
linaposagwa.

Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa
na madini mengi ambayo hayapaswi kutupwa
tu.
Lakini kampuni hiyo inakumbwa na kesi
mahakamani ambayo huenda ikaisababisha
kufungwa.
Kampuni hiyo ilishitakiwa na wataalamu
wanaohofia kuwa bidhaa hizo zinaweza kuwa
na Bakteria ambayo inaweza kusababisha
athari za kiafya kwa wanaotumia bidhaa
zinazotokana na kondo la nyuma.
Charlie Poulter, kutoka mtaa wa Reading,
anaamini kuwa alipokunywa maji ya kondo la
Nyuma pindi baada ya kujifungua ilimwezesha
kupata nguvu.
"nilikunywa harakaharaka, kwa sababu sikutaka
kutafakari kuhusu harufu na ladha yake,
alisema Charlie''
"nilikuwa nimejifungua na nilihisi kuishiwa na
nguvu sana na pia kwa kiasi kidogo
nilijidharamau. Kwa hivyo nilihisi kuwa ikiwa
nitakunywa maji hayo ingenisaidia kupata
nguvu na kupona haraka,'' alisema mama
Charlie.

Hii huwa ni kiongo cha mwili ambacho huwa
kimeshikana na nyumba ya mtoto pamoja na
kitovu.
Kiungo hicho hubeba hewa ya Oxygen na
madini kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Pia husafirisha uchafu kutoka kwa mtoto
hupitia kwa kiungo hicho hadi kwa mama.
Baada ya mtoto kuzaliwa kiungo hicho hutoka
mwilini mwa mama anaposukuma mtoto au
hutolewa na madaktari mama anapofanyiwa
upasuaji.
Binadamu kwa kawaida hajulikani kwa kula
sehemu hiyo ya uzazi. Ni kawaida kwa baadhi
ya wanyama wa baharini na wanyama wengine
wa kufugwa. Lakini kwa mwanmadamu , bila
shaka ni jambo geni.
Nchini China baadhi ya madaktari wa kienyeji
hutumia sehemu hiyo ya mwili kutengeza dawa
za kienyeji lakini utamaduni huu wa watu kula
Kondo la Nyuma umeanza tu kusikika katika
mataifa ya magharibi.
'Je wanasayansi wanasemaje?'
Hadi leo hakuna utafiti wowote kuhusu
wanawake wanaokula Kondo la Nyuma.

0 comments:

Post a Comment