Facebook

Saturday, 15 November 2014

UTAFITI TWAWEZA MAKONDA AUPINGA,AIBUKA NA HOJA YA RUSHWA

Aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Paul Makonda ameibuka na kuushangaa utafiti huo kushindwa kuuliza wananchi ni mgombea gani wa nafasi ya urais wanadhani anaweza kuongoza mapambano dhidi ya rushwa.

Makonda aliyasema hayo kufuatia utafiti uliofanywa na Twaweza kutoa matokeo bila ya kuweka swali la mgombea anayeweza kupambana na tatizo hilo licha ya asilimia 30 ya walioulizwa kulalamikia kukithiri kwa rushwa nchini.

Alisema kitendo cha asilimia 30 ya walioulizwa kulalamikia rushwa kuitafuna nchi ingepaswa sasa kuwasukuma Twaweza kuuliza wananchi hao kwa maoni yao wanadhani ni mgombea gani wa nafasi ya urais anaweza kumaliza tatizo hilo kwani ingewasaidia hata watanzania kuamua kufanya uamuzi.

"Haiwezekani asilimia 30 waseme rushwa ni tatizo halafu watafiti hao wakashindwa kuuliza swali la wanadhani ni mgombea gani nafasi ya urais anaweza kupambana na  rushwa ili kujua kama waliopendekezwa wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa Taifa kuliko kutaja majina tu ya wagombea"alisema Makonda.

Aliongeza kuwa kitendo cha utafiti huo tutohoji suala la rushwa kwa wagombea ni wazi haziwezi kuakisi ukweli wa mitazamo ya wananchi hasa katika suala la uadilifu ambayo ni moja ya sifa muhimu ya kupata viongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Makonda alisema pamoja na Bunge kutunga sheria ya gharama za uchaguzi bado matumizi makubwa ya fedha yameendelea kwenye chaguzi hivyo ilikuwa wakati mwafaka kwa taasisi hiyo kuuliza suala la uadilifu.

Chanzo:Majira

0 comments:

Post a Comment