Facebook

Friday, 14 November 2014

Watoto watatu waongea lugha ya kipekee Uganda.

Watoto watatu kutoka kijiji cha Barca
katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani Oyam
nchini Uganda wameanza kuzungumza
lugha tofauti isiojulikana baada ya
kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.
Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam
ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo
hilo.

Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia
ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.
Kulingana ma gazeti la the monitor nchini
Uganda,watoto hao hawajaathirika kiakili lakini
hawawezi kuzungumza na watu
wengine.Wanaamini tu kile baba yao
anachowaambia.

Kulingana na mama yao watoto hao waliweza
kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa
na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na
hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na
baba yao.

Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao
alimzuia kutozungumza nao hatua iliowafanya
kutojifunza lugha ya kiluo wakati walipokuwa
wadogo.

Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na
baba huyo kutosema chochote kuhusu watoto
hao.

0 comments:

Post a Comment